Baadhi
ya vibaka wakiwa wameng'oa Mashine za kutengeneza sahani na vikombe vya
udongo katika Soko la Sido Mwanjelwa ambazo hazikuharibiwa na moto
lakini wameziuza kama Vyuma chakavu, Je huu ni uungwana na tabia hii ya
kutamani fedha kwa kuuza kitu cha thamani kubwa kwa bei ndogo hali kodi
za wananchi zikinufaisha watu wachache.
Polisi walifika eneo hilo na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi
Mashine hizi nazo ziling'olewa
Vipuli ambavyo viling'olewa kwenye mashine
Hizi ni baadhi ya mashine ambazo polisi walifanikiwa kuziokoa, baada ya kufika na kuwatawanya vibaka hao kwa mabomu ya machozi
Mashine ikiwa imeondolewa swichi kubwa/Mainswitch na vibaka bila kujua thamani ya mashine hiyo.
Pia na hii ni mashione ambayo imeokolewa
Gari ambayo ilipinduliwa na kujaribu kung'olewa Injini ambapo vibaka hao hawakufanikiwa.
Watoto bila kujali moto walikuwa wakijitafutia chochote.
Bila aibu yoyote na hawa wakifika katika soko hilo lililoungua wakiwa na vitendea kazi au dhana za kukatia vyuma, kama msemeno
Mzee
huyu kwa uchungu baada ya kuunguliwa kwa banda lake akiwazuia watu
wasiingie katika eneo lake, kutokana na kuwa na baadhi ya masalia ya
bidhaa zake.
Dada
hutu mwenye asili ya China akishangaa baada ya kuvunjwa kwa chumba
chake cha biashara licha ya kuwa Moto haukuweza kufika eneo lake.
Kushoto Mama huyu akilia kwa huzuni baada ya kukuta kila kitu kimeteketea, na moto kwani alikuwa safarini..
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)