NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka watu wote wanaoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga kuacha kufanya vitendo viovu, ikiwemo kuzingatia sheria , taratibu na maadili ya uchaguzi.
Aidha tume hiyo imetoa masikitiko yake dhidi ya vitendo vya kiuhuni na visivyo vya kistaarabu vinavyofanywa na baadhi ya Vyama Vya Siasa katika uchaguzi huo. Huku ikisema kuwa viongozi wake watakwenda Igunga kuzungumza na vyama hivyo ili kuwakumbusha sheria na maadili ya uchaguzi huo.
Kauli hiyo ilitolewa leo (jana) na Mwenyekiti wa Muda wa NEC, Profesa Amon Chaligha wakati akitoa tamko la tume hiyo kuhusu kampeni
za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dares Salaam kufutia kuwepo kwa matukio mengine ya
ukwiukaji wa maadili ya uchaguzi huo.
“Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawaasa wale wote wanaofanya na wanaoendeleza
vitendo hivyo waache mara moja kwa usalama wa taifa letu na ustawi wa
wananchi wa Jimbo la Igunga kwa ujumla,” alisema Profesa Chaligha.
Aliyataja matukio
hayo kuwa ni kurushiana risasi za moto, kuwa na silaha katuika
mikutano ya kampeni, kutumia lugha za matuzi na vitisho katika mikutano
ya kampeni na kutumia lugha za kikabila badala ya Kiswahili.
Alisema
baadhi ya matukio hayo ymashawasilishwa katika kamati za maadili ya
uchaguzi ngazi ya jimbo kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ambapo yatajadiliwa na kutolewa maamuzi.
Aliongeza kuwa tume hiyo inategemea kuwa wale wote wanaoshiriki katika uchaguzi huo, na kata 22 katika halimashauri mbalimbali nchini ,wataendelea kuendesha kampeni zao kwa kuzingatia sheria za uchaguzi, maadili ya uchaguzi na maelekezo ya tume iliyotoa.
Tume
hiyo pia imesema kuwa matukio ya awali ya kumwagiwa tindikali,
kudhalilishwa kwa Mkuu wa Wilaya na kujeruhiwa kwa kukatwa mapanga
yaliwasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi huo na aliyawasilisha kwenye
kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, ambapo maamuzi yalitolewa
na kamati hiyo kuwa masuala hayo yalishafika mahakamani, hivyo mahakama
iachiwe iendelee kuyashughulikia .
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)