Madereva wa Mabasi
na Matrafiki katika Stand kuu - Mbeya.
Tukio la Madereva
wa Mabasi ya masafa marefu kutoka Mbeya kugoma kuendesha mabasi yao kwa
kulalamikia 'TOCHI' nyingi barabarani limenishangaza sana, kwa faida ya
wasioelewa, TOCHI ni Kamera za usalama barabarani zinazotumiwa na Matrafiki kuangalia magari yanayokwenda mwendo
wa kasi katika eneo ambalo hawastahili kwenda mwendo huo.
KAPINGAZ Blog
inapata shaka kidogo, ni kweli hao Madereva wanagomea TOCHI! au kuna kitu
kingine Chini ya kapeti? nadhani wao madereva wanalijua hili. Wosia wangu, kama
Madereva wanagomea TOCHI kama TOCHI isitende kazi yake, nitapingana nao kwa
asilimia 100; ila kama kuna lingine nje ya hapo nawasapoti vile vile kwa
asilimia hizo hizo.
"TAFADHALINI,
TAIFA BADO LINAZIHITAJI NGUVU HIZI ZA WATANZANIA WANAOPOTEA KILA SIKU KWENYE
AJALI AMBAZO NYINGI ZINASABABISHWA NA UZEMBE"
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)