: Dk. Padhani akiwa kazini akimfanyia upasuaji wa macho mmoja wa wagonjwa wa macho 100 wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji.
Baadhi
ya wagonjwa wa macho wakiwa kwenye dirisha la mapokezi la hospitali ya
mkoa iliyopo mjini humo kwa ajili ya kujiandakisha.
Na.Nathaniel Limu
Wagonjwa
wa macho zaidi ya mia moja (100) kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa
Singida,wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji mbalimbali ukiwemo wa kutoa
mtoto wa jicho, katika kipindi cha siku tatu mfululizo kuanzia jana
(16/9/2011).
Wagonjwa
hao ambao wanafanyiwa upasuaji na kupewa huduma ya malazi bure, zoezi
hilo linaendelea kufanyika katika wodi ya macho iliyopo katika hospitali
ya mkoa mjini Singida.
.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,kiongozi wa timu ya madaktari inayosimamia zoezi hilo, Dk.Dh.Padhani, amesema zoezi hilo linafanywa kwa ushirikiano wa pamoja
na madaktari wa macho kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili na shirika
lisilo la kiserikali la Bilali Muslim Mission la jijini Dar-es-salaam.
Amesema zoezi hilo ni nyeti,
limeadaliwa na kufadhiliwa na kampuni maarufu nchini ya jijini
Dar-es-salaam ya Mohammed Enterprises ltd ambayo mkurugenzi wake, ni
mbunge wa jimbo la Singida mjini (CCM),Mohammed Gulam Dewji.
Akifafanua
zaidi, amesema wagonjwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo, hulazwa kwa
mapumziko zaidi kwenye wodi ya wagonjwa wa macho ambayo ujenzi wake
umegharamiwa na mbunge Dewji, pamoja na wadau wa maendeleo.
Kwa
mujibu wa msaidizi wa mbunge Dewji, Hassan Mazala ambaye pia ni katibu
mwenezi wa CCM manispaa ya Singida, zoezi hilo la siku tatu,linatarajiwa
kugharimu zaidi ya shilingi milioni sita.
Mbunge
Dewji kwa kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali,kwa miaka mingi
iliyopita, amekuwa akiandaa na kufadhili shughuli mbalimbali za matibabu
ya macho kwa wananchi wa jimbo lake na mkoa kwa ujumla.
Amekuwa
akidai kwamba zoezi la upasuaji au matibabu ya macho, amekuwa akilipa
umuhimu wa aina yake kwa kuamini mtu mwenye uono mzuri, anauwezo wa
kutosha kupigana na maadui ujinga,umaskini na maradhi bila tatizo.Kwa hisani Ya Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)