SALHA ISRAEL AIBUKA KIDEDEA TAJI LA VODACOM MISS TANZANIA 2011 NA KUNYAKUA GARI JIPYA LENYE THAMANI YA SHILINGI MIL 72 USIKU WA KUAMKIA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SALHA ISRAEL AIBUKA KIDEDEA TAJI LA VODACOM MISS TANZANIA 2011 NA KUNYAKUA GARI JIPYA LENYE THAMANI YA SHILINGI MIL 72 USIKU WA KUAMKIA LEO

Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel akipunga mkono baada ya kuvishwa taji hilo Usiku wa Kumkia leo katika shindano kali lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mshindi wa Pili Tracy Mabula (kulia) na Mshindi wa tatu  Alexia Williams.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare akimpongeza Miss Tanzania 2011, Salha Israel na kumkabidhi gari yake aina ya Jeep alilozawadiwa mara baada ya kuchukua taji la Vodacom Miss Tanzania 2011.
Miss Tanzania 2011, Salha Izrael akionesha ufunguo wa gare lake jipya aina ya Jeep, lenye thamani ya sh Milioni 72 alilokabidhiwa usiku wa kuamkia leo baada ya kushinda taji la Vodacom Miss Tanzania.
Mmoja wa washiriki akiwa katika vazi la jioni usiku huu wakati wa shindano la Vodacom Miss Tanzania kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Mwimabji kutoka nchini Uganda Juliana akiimba wakati wa shindano hilo lililofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Baadhi ya warembo wakiwa katika vazi la ufukweni wakati walipokuwa wakipita jukwaani katika shindano la Vodacom Miss Tanzania kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam uskiu huu.
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakicheza katika shoo ya ufunguzi wa shindano hilo lililofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Wana Kamati kutoka Vodacom Tanzania wakiwa wametulia na kushuhudia shindano hilo mara baada ya kazi kubwa ya maandalizi ya muda mrefu ya shindano hilo, Vodacom Tanzania ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo kwa muda mrefu sasa.
 
Warembo wa shindano la Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika vazi la jioni.Picha Na John Bukuku, Father Kidevu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages