Shirikisho
la soka Tanzania (TFF) limegoma kuyatambua maridhiano ya klabu ya Yanga
na wadhamini wa kuu wa ligi Kuu ya Bara, kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom kuhusu jezi za Yanga kutokuwa na doa jekundu.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema kuwa, wanashindwa kutambua makubaliano hayo kwani kanuni za TFF ziko juu ya Yanga, hivyo kimaamuzi Yanga hawako juu ya sheria na kanuni za shirikisho hilo.

“Hata sisi hatuwezi kuwa juu ya kanuni na sheria za Shirikisho la soka
Afrika (CAF), hivyo Yanga hawawezi kuwa juu yetu kimaamuzi, kama
inawezekana makubaliano hayo yangetushirikisha kama baba wa soka
Tanzania,” alisema Wambura.
Wambura alisema wameweka wazi suala hilo ili baadaye timu nyingine zikijitokeza na matakwa ya rangi zake wadhamini wasigome kuwatekelezea matakwa hayo.
Sakata la Yanga kugomea nembo hiyo linatokana na kuwepo kwa doa jekundu ambalo Yanga wameipinga na kudai katiba yao hairuhusu kuvaa kitu chenye rangi nyekundu.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)