Na Mwandishi wa
Jeshi la Polisi-Kagera
Polisi mkoani Kagera wamemuua
kwa kumpiga risasi mmoja ya wachimba madini wadogo waliokuwa
wakijaribu kumchoma moto mwenzao mmoja aitwaye Samwel Marwa (28),
Mkazi wa Kijiji cha Runzewe, Wilaya ya Bukombe, Mkoani Shinyanga kwa
tuhuma za kuwaibia madini yao.
Kamanda wa
Polisi mkoani Kagera Henry Salewi amesema kuwa katika harakati za
kumuokoa kijana huyo pia Askari Polisi wawili wamejeruhiwa kwa
kushambuliwa kwa mawe na wachimbaji hao wa madini wakati walipokuwa
wakimuokoa mmoja ya wachimbaji hao aliyekuwa akichomwa moto kwa tuhuma
za wizi wa madini.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera SACP Henry
Salewi, amewataja Askari waliojeruhiwa kuwa walifanikiwa kumuokoa
kijana huyo, lakini Askari wawili F. 5609 D/CPL. Daniel Wangiboma na
G. 3568 PC Ntimbula Bakari walijeruhiwa kwa mawe vichwani na
wamekimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Biharamulo kwa matibabu.
Amesema siku
ya tukio hilo jana Polisi wa Kituo kidogo cha Mavota kwa kushirikiana
na Askari Polisi wa Operesheni Wilayani Biharamulo, walimuua mtu huyo
ambaye hajafahamika jina lake wakati wakiwa katika harakati za
kumuokoa kijana huyo.
Kamanda Salewi amesema kuwa,
marehemu ambaye hajafahamika jila lake, alikuwa ni miongoni mwa kundi
la wachimbaji waliokuwa wakimshikilia kijana huyo na kuwashambulia
Polisi kwa kuwapiga kwa mawe ili kutomuokoa kijana waliodai amewaibiua
madidi yao.
Kamanda Salewi amemtaja kijana
aliyetunusurika kuchomwa moto kutokana na wizo huo ambaye pia bado
anahojiwa na Polisi kuwa ni Samwel Marwa (28).
ambaye alikuwa amekamatwa na kundi la wachimbaji wadogo
wadogo wapatao 100 kwa nia ya kumchoma moto kwa madai kwamba Samwel
alikuwa amewapora dhahabu zao.
Amesema mara
baada ya kuona maisha ya kijana huyo yalikuwa hatarini, baadhi ya
wananchi walikimbia katika kituo kidogo cha Polisi cha Mavota Wilayani
Biharamulo ambapo kwa kushirikiana na askari Polisi walioko kwenye
Operation maalumu eneo la Mgodi wa Madini madini ya dhahabu wa Tulawaka
unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick, walikimbia kwenda kuokoa maisha ya
kijana huyo.
Amesema kuwa walipokaribia
kwenye kundi la watu hao, Polisi walianza kushambuliwa kwa mawe na
kujaribu kufyatua risasi hewani bila ya mafanikio na ndipo walipompiga
mmoja na kuanguka na wengine kukimbia na kufanikiwa kumuokoa kijana
huyo.
Askari hao
pia wamefanikiwa kupata mafuta lita tatu aina ya Petrol ambayo ilikuwa
itumike kwa kumchomea moto kijana huyo.
Amesema
kuwa katika tukio hilo watu wanne walikamatwa kuhusiaka na jaribio hilo
la mauaji na amewataja waliokamatwa kuwa ni Jejo Motopasi(26) Simon
Motopasi(22) na James Vicent(20) wote wakazi wa Kiji cha Runzewe
Wilaya ya Bukombe na Vicent Idian(25), Mkazi wa Kijiji cha Mavota
Wilayani Biharamulo.
|
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)