Rais Kikwete awafariji na kuwapongeza wanakijiji wa Nungwi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Rais Kikwete awafariji na kuwapongeza wanakijiji wa Nungwi

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji na kuwapongeza wananchi wa kijiji cha Nungwi kufuatia juhudi zao za kujitolea kuwaokoa watu waliopata ajali katika meli ya MV.Spice Islanders iliyotokea juzi usiku.Meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kwenda Pemba amapo watu zaidi ya 200 wanahofiwa kufa maji.Abiria 602 wameokolewa wakiwa hai.
Balozi wa Marekani nchi Tanzania Alfonso Leinhardt akimfariji Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia ajali ya meli ya Spice Islanders iliyotokea huko Nungwi, Unguja juzi usiku ambapo watu zaidi 200 wamepoteza maisha na wengine 602 kuokolewa wakiwa hai (picha na Freddy Maro).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages