Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa
katika Viwanja vya Maisala mjini Unguja, wakati alipotembelea katika eneo hilo
lililokuwa likitumika kupokelea miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli
ya Spice jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na kumpa pole
mmoja kati ya wakazi wa Unguja waliopotelewa na ndugu katika ajali ya meli ya
Spice iliyotokea eneo la Nungwi, wakati makamu alipotembelea majeruhi waliolazwa
katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua
maeneo yaliyokuwa yakitumika kupokelea na kuhifadhi miili ya watu waliokufa
katika ajali ya meli ya Spice, pamoja na majeruhi waliokuwa wakipitishwa katika
eneo hilo la Ufukwe wa Bahari ya Hindi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja
leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa
Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati walipokutana katika viwanja vya
Maisala, walipofika kutembelea mabanda ya kupokelea miili ya watu waliofariki
katika ajali ya meli ya Spice jana
Makamu
wa Rais, Dkt Bilal, akiondoka katika eneo hilo baada ya kuzungumza na wananchi
wa Nungwi na kuwapa pole na hongera kwa huduma walizotoa katika waathirika wa
ajali hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na wakazi viongozi na wakazi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja,
wakati alipofika katika eneo hilo kwa ajili ya kuwafariji wakazi hao waliopatwa
na matatizo pamoja na kukagua shughuli za uokoaji, leo.
Hata
hivyo baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kuhusiana na jitihada za Serikali na
watu binafsi katika kutoa huduma za uokoaji, ambapo walisema kuwa katika ajali
zote zilizokwishatokea haikuahi kutokea waathirika kupata huduma ya haraka kama
hii ambapo hadi vyombo binafsi vya usafiri vliliweza kuhamasika na kuelekea eneo
la tukio kutoa msaada.
Baada
ya Rais kutembele eneo la tukio leo hii, ameagiza wataalam wa DNA nao kufika
eneo hilo kwa ajili ya kuweza kutambua wale watakaokuwa wamewakosa ndugu zao
kupitia vipimo maalum Sayansi ya Vianasaba, ambapo tayari madaktari bingwa
wamekwishawasili Unguja kwa kuanza zoezi hilo.
Wakati
huo huo, wataalam wa uogeleaji na kupiga mbizi 'Wazamiaji' kutoka Afrika ya
Kusini wanatarajia kuwasili kesho eneo la tukio kwa ajili ya kuungana na
wataalam wa nchini katika kutafuta miili iliyonasa katika meli
hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)