Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kushoto) akikabidhi
msaada wa gari la kutolea huduma za tiba linalotembea (mobile
clinic) kwa Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda katika viwanja vya
Karimjee
jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwa Mafuru ni Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Said Mecki Sadiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (kulia) akimkaribisha Waziri
wa Afya, Dk Haji Mponda katika hafla ambayo benki hiyo ilikabidhi
msaada wa gari la kutolea huduma za tiba linalotembea
(mobile
clinic) kwa Waziri huyo kwa ajili ya Bodi ya Afya Mkoa wa Dar es
Salaam jijini humo leo. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Jerome
Ringo na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki
Sadiki.
Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda akikabidhi funguo za gari la Mobile Clinic
lililotolewa msaada na benki ya NBC kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Afya
Mkoa wa Dar es Salaam , Jerome Ringo jijini Dar es Salaam leo.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki.
Baadhi wa maofisa wa NBC na wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini
hafla ya makabidhiano ya gari la Mobile Clinic lililotolewa msaada na
benki ya NBC kwa Bodi ya Afya Mkoa wa Dar es Salaam katika
Viwanja vya Karimjee jijini humo leo.
Viwanja vya Karimjee jijini humo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki (kushoto) akifurahi
na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru katika hafla ambayo
benki hiyo ilikabidhi msaada wa gari la kutolea huduma za tiba
linalotembea (mobile clinic) kwa Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda (hayupo pichani) katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
linalotembea (mobile clinic) kwa Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda (hayupo pichani) katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Wacheza ngoma wa kikundi cha Makumbusho Cultural Troupe wakitoa burudani
katika hafla ya makabidhiano ya gari la Mobile Clinic lililotolewa
msaada na benki ya NBC kwa Bodi ya Afya Mkoa wa Dar es Salaam katika
Viwanja vysa Karimjee jijini humo leo.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)