MKURUGENZI wa Uchaguzi jimbo la Igunga Magayane Protace (kulia)
akimkabidhi fomu za kuwania ubunge wa jimbo hilo, mgombea mteule wa CCM
Dk. Dalally Kafumu , jana. Wengine ni Katibu wa CCM wilaya ya Igunga
Neema Adamu na Msimamizi wa masuala ya uchaguzi wa CCM, Matson
Chizi.(Picha na Bashir Nkoromo)
MGOMBEA mteule wa CCM jimbo la Igunga Dk. Dalally Kafumu (kushoto) na
Mratibu wa Uchaguzi wa CCM jimboni humo, Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na
Fedha Mwigulu Nchemba wakiwa katika huzuni kwenye hospitali ya wilaya
ya Igunga ambako walisaidia kupeleka mwili wa mtoto Peter Ezekiel
ambaye alifariki papo hapo baada ya kugongwa na lori la mizigo katika
barabara ya Igunga-Singida akijarbu kuvuka barabara akiwa na mamia ya
wananchi wa jimbo hilo waliokuwa wakimsubiri Kafumu na msafara wake,
jana. Kulia ni ndugu wa mtoto huo. (Picha na Bashir Nkoromo).
MGOMBEA
mteule wa CCM jimbo la Igunga Dk. Dalally Kafumu (kushoto) na Mratibu
wa Uchaguzi wa CCM jimboni humo, Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha
Mwigulu Nchemba wakimfariji Kulwa Mpina baada ya kufukisha kwenye
chumba cha kuhifadhi maiti mwili wa mtoto Peter Ezekiel ambaye
alifariki papo hapo baada ya kugongwa na lori la mizigo katika barabara
ya Igunga-Singida akijarbu kuvuka barabara akiwa na mamia ya wananchi
wa jimbo hilo waliokuwa wakimsubiri Kafumu na msafara wake, jana.
(Picha na Bashir Nkoromo).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)