Dr Mary
Mwanjelwa akiwakabidhi Maafisa wa gereza la Ruanda.
Dr Mwanjelwa
akiwa na Maafisa mbalimbali wa Gereza la Ruanda nje ya bwalo la Maafisa
hao.
Na mwandishi wetu.
Mbunge wa viti maalum wanawake kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Mbeay Dk Mary Mwanjelwa
ametembelea wafungwa katika gereza la Ruanda lililopo jijini Mbeya
katika mfululizo wa ziara zake mkoani hapa.
Mheshimiwa
Mwanjelwa katika ziara yake kwenye gereza hilo alitembelea maeneo
mbalimbali kama vile sehemu za jiko, malazi pia zahanati ndogo ya gereza
hilo ambapo mkuu wa gereza hilo ACP Mbunda alimtembeza maeneo hayo na
baadae kuongea na na wafungwa hao na kushirikiana chakula katika gereza
hilo.
Wakieleza
baadhi ya kero gerezana hapo Mkuu wa gereza ACP Mbunda
alisema baadhi ya wafungwa wamefungwa kwa makosa mbalimbali ambayo
mengine yangeweza kuzungumzika mtaani na wengine kushindwa kupata nakala
za hukumu.tangu mwaka 1996 hali ambayo hali inayopelekea mrundikano wa
wafungwa katika gereza hilo.
Kwa upande wake
Mbunge wa viti Maalum Dk Mwanjelwa aliwashukuru askali hao kwa moyo wa
uvumilivu kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na kuwaasa kuwa
serikari inayatambua matatizo yao na kwamba inawafanyia kazi hivyo
wasife moyo kwa serikali inawajali watumishi wake.
Aidha Dk
Mwanjelwa aliwaahidi kuwa kero zao itazifikisha sehemu husika na
alikubaliombi lao la kupatiwa kungiamuzi cha runinga ambacho waliomba
katika risala yao iliyosomwa kwake na mmoja wa wafungwa gerezani hapo.
Akihitimisha ziara yake katika
gereza hilo Mbunge huyo wa viti maalum mkoani Mbeya alitoa zawadi
mbalimbali kwa wafungwa hao yakiwemo mafuta ya kupakaa na sabuni za
kufualia ambapo mbunge huyo alisema waupokee kwa moyo msaada huo kama
ishara ya upendo kwao kwani magereza suio mahali pa adhabu bali ni
mahali pa kurekebisha mtu tabia ingawa wengine wamefikishwa hapo kwa
kuonewa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)