Rais mpya wa Zambia
Mh. Michael Sata.
Rais wa Kenya Mwai
Kibaki.
Naomba wachambuzi
wa mambo ya Siasa na wana Demokrasia na Diplomasia waweze kunisaidia hili,
wengi wa viongozi wetu wa Kiafrika mara wanapotangazwa kuwa wameshinda katika
chaguzi zao hukimbilia kuapishwa mapema.
Hii inaashiria
nini! kutokujiamini? Hamu ya Madaraka? Kuwapenda sana wananchi wake? ni sehemu
tu ya utaratibu wa kila mgombea ambaye ameshinda au ni shinikizo tu kutoka nje
ya Taifa lake? Naomba wachambuzi wanisaidie hili.
Kwa upeo wangu
mdogo naamini kama nchi ambayo ina Demokrasia ya ukweli na wananchi wake
wameandaliwa vizuri kuidumisha hiyo demokrasia, sioni sababu ya kiongozi ambaye
ameshinda kwa haki kukimbilia kuapishwa haraka.
KAPINGAZ Blog
inasema, WANASIASA JENGENI UWEZO WA KUJIAMINI NA WAFUNDISHENI WANANCHI WENU
DEMOKRASIA YA KWELI HATA UONGOZI WENU UTAKUWA WA HURU, HAKI NA USAWA.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)