Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa mhadhara na kuelezea uzoefu wa Tanzania kuhusu changamoto za
sayansi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za
Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Sweden. Mhadhara huo
uliambatana na safari ya Makamu wa Rais katika maabara mbalimbali
zilizopo chuoni hapo jana Sept. 26, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Uppsala Sweden, Bo Sundavist (katikati)
na Mkurugenzi, Romain Murenzi, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ua
Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo
nchini Sweden. Mhadhara wa maadhimisho hayo ulifanyika jana Sept. 26
nchini hapa.
MamaAsha Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa Chuo cha Uppsala, Mikael
Norrby, kuhusu Viumbe vilivyokaushwa na kuhifadhiwa
katika Jumba la makumbusho la Gustavo Adolpho nchini Sweden,
wakati Mama Asha alipotembelea katika Jumba hilo na kujionea mambo
mbalimbali ya kisayansi yaliyomo katika Jumba hilo jana sept. 26.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)