Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Maiti zilizopatikana hadi sasa ni 192 na watu 601 wameokolewa wakiwa
hai katika eneo la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja kati ya watu 760
waliosajiliwa kusafiri na meli ya MV Spice Islander iliyokuwa ikielekea
kisiwani Pemba jana usiku wa Septemba 9, 2011.
Baadhi ya Abiria walionusurika walisema kuwa
abiria walijaa kupita kiasi katika Meli hiyo kongwe ya MV Spice
Islander iliyokuwa ikielekea Pemba.
MV Spice Islander ilianzia safari yake kwenye
Bandari ya Dar es Salaam ambapo iliondoka mchana wa Septemba 9, 2011
ikielekea Pemba kupitia Zanzibar.
Ingawa haijafahamika maramoja kuwa Dar es
salaam iliondoka ikiwa na abiria wangapi na mizigo yenye tani ngapi,
lakini meli hiyo ilitia nanga kwenye Bandari ya Zanzibar na kuondoka
kuelekea Pemba usiku wa kuamkia Septemba 10, 2011 ikiwa na abiria 670
waliosajiriwa.
Mnamo majira ya saa 7.30 usiku meli hiyo ikiwa
katika eneo la Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja ilianza kupinduka
polepole na hadi ilipofika saa 9.00 usiku meli hiyo ilipinduka na
hatimaye kuzama kabisa kwa kuelemewa na mizigo pamoja na abiria.
Baadhi ya wananchi wameitupia lawama malka ya bandari na
Sumatra kwa kushindwa kudhibiti uchukuzi wa abiria na mizigo kupita
kiasi.
Kazi ya utafutaji wa watu walio hai na uopoaji
wa maiti bado unaendelea na vikosi vya Jeshi la Polisi wanamaji, KMKM
na JKU wanaendelea na kazi hiyo.
Jeshi la Polisi limetuma timu ya wataalamu wa
Upelelezi na Madaktaji pamoja na Meli moja ya uokoaji MV Mamba ikiwa na
boti nyingine ndogondogo ziendazo kasi za msaada majiuni.
Serikali ya Zanzibar na ile ya Muungano
kupitia marais JK na Dk. Shein wametangaza siku tatu za maombolezo
kuanzia kesho Septemba 11, 2011 na bendera zote zitapepea nuzu
mlingoti.
Hakutakuwa na sherehe zozote ama mikusanyiko
yenye kuonyesha buurudani na michezo.
Mh. Zito Kabwe,
yeye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na
Waziri Kivuli wa Fedha, alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa vyama vya
Siasa waliofika katika viwanja vya Maisala mjini Zanzibar na kutoa Pole
kwa wafiwa na kusema Chama chake kimesitisha kwa muda shughuli za
kampeni katika jimbo la Igunga mkoani Tabora kutokana na msiba huo
mzito.
Hiyo ni meli ya pili kuzama baharini ikiwa
safarini kuelekea Pemba na meli ya kwanza ilikuwa ni MV Fatahi
iliyozama mwaka jana 2010 ikiwa Bandari ya Zanzibar ikielekea Pemba.
Meli nyingine mbili ziliungua moto zikiwa
bandarini Zanzibar na meli nyingine ya MV El- Salaam ilizama Baharini
ikiwa na bidhaa mbalimbali ikielekea Songosongo Kilwa kwenye utafiti wa
mafuta.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)