KILIMANJARO PREMIUM LAGER NA BONGO 5 MEDIA ZAWAKUTANISHA WASANII WATAKAOTUMBUIZA KATIKA TAMASHA LA BIA TANZANIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KILIMANJARO PREMIUM LAGER NA BONGO 5 MEDIA ZAWAKUTANISHA WASANII WATAKAOTUMBUIZA KATIKA TAMASHA LA BIA TANZANIA


Dar es Salaam Septemba 29, 2011- Wasanii zaidi ya kumi watakaotumbuiza katika Tamasha la kwanza la Bia Tanzania Jumamosi na Jumapili katika Viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam wameahidi kutoa burudani ya aina yake kwa watanzania.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wasanii hao na wawakilishi waliishukuru Bia ya Kilimanjaro Premium Lager na Kampuni ya Bongo 5 kwa kuandaa tamasha hili kubwa la kwanza na la aina yake Mkoani Dar es salaam, 
Baadhi ya wasanii na makundi yaliyohudhuria mkutano huo na waandishi wa habari ni Chidi Benz, Msondo Ngoma, Twanga Pepeta, Akudo Impact, Canal top, Tip Top, Ben Paul, Linex, Linah na THT ambao waliwapa wandishi wa habari vionjo kidogo ya vitu ambavyo watavifanya katika tamasha hili.

Kilimanjaro Premium Lager ikishirikiana na Kampuni ya Bongo 5, Alliance Francaise na Taasisi ya Goethe wanandaa tamasha kubwa la bia la kwanza Tanzania ambalo litafanyika katika Viwanja vya Leaders Octoba 1 na 2 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages