Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kulia) na Rais wa Rotary Club Mikocheni,
Irene Kamau wakikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi kisima cha maji
chenya matanki mawili ya kuhifadhi lita 10,000 za maji kwa Kituo cha
Afya ya Uzazi cha Mbagala Round About, Temeke, Dar es Salaam juzi.
Anayeshuhudia kushoto ni Daktari Mkuu Mfawidhi wa kituo hicho, Batuli
Luhanda. Kupitia Rotary hiyo TBL ilifadhili mradi huo kwa gharama y ash.
Milioni 9.
Wanachama wa
Rotary Club Mikocheni, wakiongozwa na Rais wao, Irene
Kamau ( wa pili kulia) wakimshukuru Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), baada ya ya kukabidhi kwa Kituo
cha Afya ya Uzazi cha Mbagala Round About, Temeke Dar es Salaam juzi,
mradi wa kisima cha maji chenye matanki mawili ya kuhifadhia lita
10,000 kilichojengwa kwa ufadhili wa TBL kwa gharama ya sh. Milioni 9.
(Wapili ushoto ni, Daktari Mkuu Mfawidhi wa kituo hicho, Batuli Luhanda.
Rais wa
Rotary Club Mikocheni, Irene Kamau (kulia) na Daktari Mkuu Mfawidhi wa
Afya ya Uzazi cha Mbagala Round Abaout, Batuli Luhanda (
wa pili kulia), wakimshukuru Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), Dorris Malulu (kushoto), baada ya kukabidhi kwa kituo hicho,
mradi wa kisima cha maji chenye matanki mawili ya kuhifadhia lita
10,000 kilichojengwa kwa ufadhili wa TBL kwa gharama y ash. Milioni 9.
Daktari Mkuu
Mfawidhi wa Kituo cha Afya ya Uzazi cha Mbagala Round About, Temeke, Dar
es Salaam, Dk. Batuli Luhanda (kushoto), akitoa shukrani kwa Kampuni ya
Bia Tanzania (TBL) na Rotary Club Mikocheni kwa kuwezesha ujenzi wa
kisima cha maji chenye matanki mawili ya kuhifadhia lita 10,000 za maji
katika kituo hicho. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu
aliyekabidhi kisima hicho juzi, kilichojengwa kwa gharama ya sh. Milioni
9 zilizotolewa na TBL kufuatia maombi ya Rotary hiyo.
Mama Mkazi wa
Mbagala, Daima Ahamad aliyejifungulia mtoto katika Kituo cha Mbagala,
Round About, akitoa shukrani kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na Rotary
Cub Mikocheni, kwa kuwezesha ujenzi wa kisima cha maji chenye matanki
mawili ya kuhifadhiwa lita 10,000 za maji. Kisima hicho ambacho ujenzi
wake uligharimu sh. Mil. 9 zilizotolewa na TBL kilikabidhiwa kwa uongozi
wa kituo hicho juzi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)