KAMPUNI YA BIA NCHINI TBL YACHANGIA HARAMBEE YA MAABARA,GARI ST MARY'S MOSHI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KAMPUNI YA BIA NCHINI TBL YACHANGIA HARAMBEE YA MAABARA,GARI ST MARY'S MOSHI


Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Mkoa wa Kilimanjaro, Leiya Hermenegild (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.mil.10, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St. Mary Goretti ya mjini Moshi, Mtawa Lucretia Njau. Fedha hiyo ilitolewa na TBL kuchangia fedha za kusaidia kunua vifaa vya maabara na gari la shule hiyo. Hafla hiyo ilifanyika juzi wakati wa mahafali ya shule hiyo, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya ambaye pia nia Mwenyekiti wa Bodi ya TBL.
Meneja wa Shule ya Sekondari ya St. Marry Goretti, Mtawa Fina Mushi na Mkuu wa shule hiyo Mtawa Lucretia Njau wakimkabidhi zawadi ya kikombe Waziri Mkuu mstaafu,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Cleopa Msuya (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 10 ya kidato cha nne yaliyofanyika juzi katika shule hiyo, iliyopo Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. TBL ilichangia sh. mil. 10 katika harambee ya ya kununulia vifaa vya maabara na gari la shule.
Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mary Goretti, mjini Moshi, wakati wa mahafali ya kumi ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo juzi, ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi. TBL ilitoa msaada wa sh. mil. 10 za kusaidia kununua vifaa vya maabara na gari la shule hiyo.
Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (kushoto) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akipatiwa zawadi ya picha na wanakamati wa mahafali ya kumi ya Shule ya Sekondari ya St. Mary Goretti ya mjini Moshi juzi,kwa  kutambua mchango wake wa maendeleo  katika Taifa. katika mahafali hayo ambayo Msuya alikuwa mgeni rasmi, TBL, ilitoa msaada wa sh. milioni 10 za kusaidia kununua vifaa vya maabara na gari la shule hiyo.
Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (kushoto) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akipatiwa maelezo na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mary Goretti ya mjini Moshi juzi, kuhusu matumizi ya vifaa vya maabara wakati wa mahafali ya kumi ya shule hiyo.Katika mahafali yaliyofanyika sambamba na harembee, TBL ilichangia sh. mil. 10 za kusaidia kununua vifaa vya maabara na gari la shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages