Jumuiaya ya Watanzania nchini Uingereza TANZ-UK
ikishirikiana na TANZ-UK Jumuiya ya Wanzanzibar
waishio Uingereza (ZAWA) Urban Pulse na Miss Jestina George Blog imeandaa fundrising maalum kwa ajili ya kuweza kuwasaidia
waathirika wa ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea Nungwi njiani
kuelekea Pemba. Fundrising hii itafanyika katika Ubalozi wetu hapa
London tarehe 17 Septemba 2011 Kuanzia saa nane mchana.
Tunawaomba Watanzania wote mlioko hapa nchini Uingereza
kutoka jumuiya mbalimbali,vyama vya kisiasa, wafanyabiashara, wanafunzi
na hata wasio Watanzania mjitokeze kwa wingi ili kuweza kujumuika nasi
na kufanikisha zoezi hili. Hivyo basi tunaomba mwenye fedha au
chochote kile cha kuweza kuthamanishwa tunaomba tuweze kuja nacho na
kitafanyiwa mnada. Mfano, wenye biashara wanaweza wakaleta bidhaa kiasi
ambazo zitafanyiwa mnada ambapo ziada itakayopatikana itakuwa sehemu
ya mfuko tutakaokuwa tunautafuta.
anwani ni; 3 Stratford Place, London, W1C 1AS. Muda ni
saa nane mchana (2pm sharp).
Kwa maelezo zaidi tunaomba uwasiline na ...............
Mwenyekiti Tanz-UK 07766856565, ZAWA 07538063536,TA London 07404332910
UKIONA TANGAZO HILI TAFADHALI
MTAARIFU NA MWENZAKO. WOTE TUNAKARIBISHWA,
Mungu ibariki Zanzibar, Mungu
ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa . Zaidi sana Mungu wabariki
Watanzania wote popote pale walipo duniani.
ASANTENI
MWENYEKITI,
TANZ-UK
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)