Mwenyekiti
wa umoja huo Kanda ya Kaskazini, Rashid Salehe (katikati), akihutubia
mkutano wa madereva. Kulia ni Katibu umoja huo Mkoa wa Kilimanjaro,
Shaban Ramadhani na Mwenyekiti Mkoa wa Kilimanjaro Apolinary Mallya
(kushoto).
Na Joseph Ngilisho, Arusha
UMOJA wa madereva wa magari makubwa mkoa wa Arusha umeungana na wenzao wa Tunduma kwa kuandaa mgomo wa nchi nzima baada ya tarehe 30 mwezi huu iwapo serikali itashindwa kutoa ufumbuzi na mustakabali wa madai yao.
Akizungumza kwenye kikao cha pamoja cha madereva hao kilichoandaliwa mahususi kwa ajili ya kujiweka tayari na mgomo huo ambacho kilichofanyika katika shule ya msingi Mwangaza, Ngarenaro, jijini Arusha, mwenyekiti wa kanda wa umoja huo, Rashidi Salehe, alisema kuwa mgomo huo wa nchi nzima hautakuwa na kikomo, kwani alisema wamevumilia muda mnrefu manyanyaso kutoka kwa matajiri wao.
Aidha alisema sababu kubwa ya mgomo huo ni kuishinikiza serikali iwabane waajiri wao ili watambue mikataba yao ya kazi, ajira, posho za kujikimu wanaposafiri nje ya nchi wakitaka walipwe kwa dola badala ya shilingi za Kitanzania, fedha ambayo walidai wanapofika nchi nyingine na kuibadilisha huwa fedha kidogo.
Madai mengine ni kupunjwa kwa posho za kutoka mkoa mmoja kwenye mkoa mwingine ambapo walidai kwamba wamekuwa wakilipwa shilingi 20,000 hadi elfu 25,000 kwa siku badala ya shilingi 65,000 na posho ya kwenda nje ya nchi wanataka ilipwe dola 76 kwa siku.
Naye mwenyekiti wa umoja wa madereva mkoa wa Kilimanjaro, Apolinary Mallya aliwataka madereva hao kujenga umoja madhubuti utakao wasaidia kudai na kupata haki zao za msingi bila kuleta vurugu wala maandamano.
Hata hivyo aliwataka madareva hao kupunguza anasa hususani ulevi na ngono wanapokuwa wamekabidhiwa magari kwani hayo yamekuwa yakichangia katika uzembe na kuongezeka kwa ajali.Source:Global Publishers Tz

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)