NA NAFISA MADAI-MAELEZO
ZANZIBAR
TANI 80 za
mwani mkavu zilizokuwa tayari kusafirishwa kuelekea Unguja na gari
aina ya Canter Mitsubishi inayobeba mzigo zimetumbukia katika gati ya
bandari ya Mkoani Pemba.
Akizungumza
mwandishi wa habari hizi Mkurugenzi Shirika la Bandari Pemba, Hamad
Salim Hamad alisema gari hiyo ilitumbukia baharini ilipokuwa ikirudi
nyumba kujiweka sawa tayari kushusha tani za mwani huo.
Kwa mujibu
wa Mkurugenzi huyo, alisema mwani huo ulikuwa unataka kupakiwa katika
meli ya Mv. Jitihada tayari kuja Unguja na kusafirishwa nje ya nchi.
Alisema
kuwepo kwa gari chini ya maji katika gati hiyo, imekuwa ikisababisha
kuzuia meli yoyote kufunga gati hali ambayo inadhorotesha utendaji na
kulitia hasara shirika hilo.
Hamad
alisema gati ya Mkoani haina mashine ya kubebea vitu vizito ‘creen’,
ambapo tagi ya shirika hilo kutoka Unguja imetumwa kwenda kuiopoa gari
hiyo ili kuipa nafasi gati hiyo iendelee na shughuli zake kama kawaida.
“Hatuna
budi kujitolea kugharamia uokoaji wa gari hiyo kwani kuwepo kwake
kumekuwa kukidhorotesha shughuli za gati na kuifanya kupata
hasara”,alisema Hamad.
Mkurugenzi
huyo alifahamisha kuwa kutumbukia kwa gari hiyo kumetokana na makosa
ya dereva aliyekuwa akiliendesha kwa kutokuwa muangalifu wakati
akiirejesha nyumba.
Alisema marobota ya mwani huo mkavu yalinunuliwa na
kampuni ya Sea Weeds, ambapo mara baada ya zoezi la uokoaji kukamilika
shirika litakaa na kampuni hiyo ili kujadili hasara.Kwa Hisani Ya John Bukuku - Full Shangwe Blogu






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)