Mheshimiwa
Dk Mary Mwanjelwa ambaye ni Mbunge wa viti maalum mkoani Mbeya
akikabidhi Vyombo vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni 15, kwa
Kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la Kusin Magharibi, Ushirika wa
Ruanda Jijini Mbeya. Kulia aliyevalia Joho jeupe ni Mwenyekiti wa Kanisa
hilo Mchungaji Nosigwe Buya ambaye alipokea vyombo hivyo
Wanakwaya wakipiga vyombo walivyokabidhiwa na Dk Mwanjelwa.
Bwana
Mboka Mjafula aliyeinama na kulia ni Sifael George wakirusha matangazo
ya moja kwa moja ya Ibada hiyo kupitia kituo cha Baraka FM Radio ambayo
inamilikiwa na kanisa hilo.
Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Mchungaji Buya akimtambulisha Dk Mwanjelwa mbele ya waumini wa kanisa hilo
Kwaya kuu iliyokabidhiwa vyombo
Mchungaji Buya ambaye ni Mwenyekiti wa kanisa hilo akihubiria waumini Neno la MUNGU
Maandamano yakiongozwa na Makamu
Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Mchungaji Zacharia Sichone, ambayo
yalianzia katika nyumba ya mchungaji Kanisa la Moravian Ruanda na
kuelekea Kanisani.
Hii ni kamati iliyoratibu
upatikanaji wa vyombo hivyo vya muziki kutoka jijini Dar es salaam wa
kwanza kushoto ni Bwana Jacob Mwasanga, anayefuatia Charles
Mwakyusa(Bwana Mipango), Katibu ni huyo Binti wenye sketi ya Pink Grady
Mwasalemba.
Kwaya ya vijana Ruanda
Kwaya ya NLC kutoka Kiwila wilaya ya Tukuyu ambao walialikwa katika sherehe za uzinduzi wa vyombo hivyo.
Dk Mwanjelwa katikati akiwa na akiwa na Mwenyekiti wa soko la Sido Mwanjelwa lililoungua Bwana Charles Syonga.
Dk Mwanjelwa akiingia katika ibada.
Zoezi la uimbaji wa nyimbo kutoka kwenye vitabu ukaanza.
++++
Na mwandishi wetu.
Mbunge
wa viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya Dakta Mary
Mwanjelwa amekabidhi msaada wa vyombo vya muziki vyenye thamani ya
shilingi milioni 15 ambapo alichangia milioni 4 kwa wanakawaya wa kanisa
la Moroviani usharika wa Ruanda Mbeya.
Dakta Mwanjelwa amesema msaada huo ameutoa ili kuiwezesha kwaya hiyo kuongeza nguvu ya kuhubiri Neno la Mungu kupitia uimbaji.
Pamoja na misaada hiyo pia
Dakta Mwanjelwa ametoa misaada ya vitanda na magodoro kwa hospitali ya
wilaya zilizopo mkoani hapa ili kuboresha huduma za afya hasa kwa
wanawake wajawazito.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)