Dkt Shein aendelea na ziara ya kuwapa pole wananchi wa Pemba - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Dkt Shein aendelea na ziara ya kuwapa pole wananchi wa Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Wingwi Wilaya ya Micheweni Pemba,waliofiliwa na jamaa zao waliofariki kwa ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,hivi karibuni iliyotokea katika mkondo wa Nungwi.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mama Mwanamwema Shein,akiwapa pole wananchi wa Wingwi Pemba,akiwa katika ziara maalum ya kuwapa pole wananchi waliofiliwa na jamaa zao,katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander,iliyozama hivi karibuni katika mkondo wa Nungwi.
Wananchi wa Michweni wilaya ya Micheweni wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed shein,akiwapa pole kutokana na ajali ya meli ya Mv Spice islander na kusababisha vifo vya jamaa zao,katika ukumbi wa mikutano skuli ya Micheweni.
Naibu Waziri wa Afya Mhe,Sira Ubwa Mamboya,nae alipata muda wa kuwapa pole wananchi wa Wingwi Pemba,waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya meli ya Mv Spice islander hivi karibuni.Picha Na Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages