SHIRIKA la utangazaji la Ujerumani (Deutsche Welle)
Limeendelea kuimarisha huduma zake nchini Tanzania kwa kuungana na
Vodacom Tanzania kwa kurusha kipindi cha ‘Learning by Ear” kwa njia ya
simu.
Kuanzia Septemba nane mwaka huu,
hadithi fupi maarufu ya redio inayorushwa na DW, inayojulikana kama
“Learning by Ear”, itapatikana kwa mahitaji kwa watumiaji wa huduma za
simu.
Programu hii inawalenga vijana ambapo
inatoa elimu juu ya masuala ya UKIMWI, haki za binadamu, demokrasia, na
mazingira ikiambatana na simulizi na makala mchanganyiko za kisisimua
na kuburudisha.
Learning by Ear inatolewa katika luga
zote zinazotumika katika programu za radio hiyo inayolenga wasikilizaji
wa kiafrika. Tayari inarushwa hapa Tanzania kama majawapoza programu za
DW-RADIO/Kiswahili.
Deutsche Welle’s kwa Kiswahili ni
kati za programu za radio hapa nchini, ambapo inakadiriwa kuwa takiriban
silimia 70 ya watanzania wanafahamu Deutsche Welle radio na kila
theluthi moja ni msikilizaji wa mara kwa mara wa programu za Kiswahili
zinazo rushwa na radio hii.
Mbali na kurusha matangazo yake kwa
luga ya Kiswahili, radio hii pia hutoa habari kwa njia ya ujumbe fupi
(sms-news) za kila siku kupitia simu za mkononi, tovuti iliyosheheni
habari nyingi muhimu (www.dw-world.de/kiswahili), mtandao wa kijamii kama
Twitter na Facebook.
Wateja wa Vodacom ambao wamejiunga na
huduma ya “Music Radio”, kutoka Vodacom Tanzania, wanaweza wakapata
sehemu zote za kipindi cha “Learning by Ear” kwa bei ya kipekee
itakayotegemea matumizi kwa sekunde.
Wateja watatakiwa kupiga namba 09011
22 201 kwenye simu zao ili kupata huduma ya ‘music services’ na
watatakiwa kusikiliza maelekezo ya namna ya kupata mitiririko mbalimbali
ya vipindi cha ‘Learning by Ear ’.
Learning
by Ear ilianzishwa kama kipindi cha Deutsche Welle mwaka 2008 kwa
Afrika, kwa ushirikiano na Ofisi ya kimataifa ya mambo ya nje ya
Ujerumani, na ni moja ya vipindi vilivyofanikiwa sana kwa wasikilizaji
vijana.
Kipindi
hicho kwa sasa kinazalishwa kwa ushirikiano na marafiki walioko Afrika
na kuandikwa na Wahariri wa kiafrika.
Zaidi ya vituo vya radio 270 kutoka
Nchi mbalimbali za Afrika zinarusha kipindi hicho tangu kianzishwe mwaka
2008, na kukifanya kupata tunzo nyingi ikiwamo ile ya ‘kipindi chenye
ubunifu wa juu kwa Radio’ ya mwaka 2009 kutoka Chama cha Kimataifa cha
Utangazaji(AIB).
Deutsche
Welle ni kituo cha utangazaji cha Ujerumani,ikiwa na vituo kama DW-TV,
DW-RADIO na DW-WORLD.DE, zote zikiwa zinazalisha habari, kuangalia
tamaduni mbalimbali duniani kote na kuandaa midaalo ya kubadilishana
tamaduni.
Vodacom
Tanzania Ltd ni kampuni ya mtandao wa simu inayotoa huduma za
mawasiliano ya GSM kwa wateja zaidi ya milioni 9 nchi nzima kwa sasa.
Hivi karibuni Vodacom ilizindua
huduma ya haraka ya Radio na Tv kwa njia ya simu, kwa kutumia mtandao
mpana ilionao nchi nzima na bado kampuni inaendelea na tafiti kwa ajili
ya huduma zitakazowanufaisha watanzania zaidi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)