Zaidi ya watu mia moja wamekufa
baada ya bomba la mafuta kupasuka na kulipuka katika katika mji mkuu wa
Kenya Nairobi, polisi wamesema.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la viwandani la
Lunga Lunga na askari wa zima moto walipambana na moto mkali ambao
ulikuwa ukitishia makazi ya watu mjini humo.
Bomba hilo la mafuta limepita katika makazi ya
watu wengi kwenye mitaa ya mabanda katikati ya mji wa Nairobi na Uwanja
wa ndege.
Zaidi ya majeruhi 100 wamepelekwa hospitali,
maafisa wanasema.
Msemaji wa magari ya huduma za dharura alisema
waathirika wengi waliungua kiasi cha kutokufatambulika.
Taarifa zinasema mlipuko huo huenda
umesababishwa na kishungi cha sigara kilichotupwa katika mtaro wa maji
ambao ulikuwa ukielea mafuta.
Mafuta hayo yalivuja kutoka kwenye tangi moja
katika ghala linalomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Kenya, msemaji wa
polisi Charles Owino ameliambia shirika la habari la Reuters.
‘Miili yaelea’
Polisi na jeshi wameweka vizuizi katika eneo
hilo, ambapo wakazi walisema kuvuja kwa mafuta kwenye bomba hilo na
kusababisha watu wengi kukimbilia kuchota mafuta yaliyovuja. "Kulikuwa na sauti kubwa ya mlipuko, mlipuko
mkubwa, na moshi na moto ukiwaka juu angani," mkazi mmoja Joseph Mwego
aliliambia shirika la habari la AFP.
Sehemu ya miili ilionekana ikiungua kiasi cha
mita 300 (futi 1,000) karibu na eneo la tukio, wenyeji walisema. Miili mingine likuwa inaelea katika mto karibu
na eneo hilo ambapo watu walioungua iliripotiwa waliruka baada ya
kushika moto.
Vibanda vilivyoezekwa kwa mabati vimejengwa
karibu kabisa na bomba hilo, wakazi walisema. Kumekuwa na vifo vingine ambavyo vimetokana na
watu kuchota mafuta yanayovuja: Zaidi ya watu mia moja walikufa eneo la
Molo, magharibi mwa Kenya mwaka 2009 baada ya lori la mafuta kupinduka
na moto kulipuka.Source BBC Swahili
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)