Balozi Amina Salum Ali Anaugana na Watanzania Wote Kuomboleza Maafa ya Watanzania Wenzetu Yaliyosababishwa na kuzama kwa meli ya Spice Islanders - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Balozi Amina Salum Ali Anaugana na Watanzania Wote Kuomboleza Maafa ya Watanzania Wenzetu Yaliyosababishwa na kuzama kwa meli ya Spice Islanders


Balozi Amina Salum Ali
--
Mwakilishi wa Umoja wa Afrika (African Union) Balozi Amina Salum Ali kwa niaba ya Umoja wa Afrika nchini Marekani, anaungana na Watanzania wote popote duniani, kuomboleza kutokana na maafa ya Watanzania wenzetu yaliyosababishwa na kuzama kwa meli ya Spice Islanders usiku wa kuamkia leo katika mkondo wa Nungwi, Kaskazini mwa kisiwa cha Unguja. Aidha, Balozi Amina Salum Ali anawapa pole wale wote waliofikwa na msiba huu mkubwa na kumwomba Mungu awafariji wale wote waliofikwa na tukio hili la kusikitisha.

Mwenyezi Mungu andelee kuwapa unafuu wa kiafya wale waliojeruhiwa katika tukio hili na pia azilaze roho za wale wote waliopoteza maisha yao mahali pema peponi, Amina.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages