Wachezaji wa Al Ahly
Mabingwa mara sita wa soka
barani Afrika Al Ahly wametolewa katika mbio za Ligi ya Ubingwa wa
Afrika baada ya kwenda sare ya 1-1 na Esperance ya Tunisia katika
mchezo wa mwisho wa kundi B.
Wydad imemaliza ikiwa imevuna pointi saba mbele ya mabingwa hao wa Misri kwa tofauti ya mabao ya kufunga. Matokeo ya mwisho yatajulikana siku ya Jumapili wakati Enyimba ya Nigeria itaikaribisha Cotonsport ya Cameroon na Al Hilal ya Sudan itakapokuwa wageni wa Raja Casablanca ya Morocco.
Enyimba tayari imekwishafuzu, ikiiacha Coton Sport na Al Hilal kupigania nafasi ya pili wakati Raja Casablanca itakamilisha mkiani.
Source: BBC SWAHILI





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)