WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI ILIPOWASILISHA BAJETI YAKE HAPO JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI ILIPOWASILISHA BAJETI YAKE HAPO JANA

          Waziri SAMWEL SITTA akiwa na TUNDU LISSU
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewasilisha Bajeti yake ya mwaka 2011/2012 ambapo imetaja vipaumbele tofauti ikiwemo kuweka mkakati utakaosaidia kukuza biashara baina ya Tanzania na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akiwasilisha Bajeti hiyo Bungeni mjini Dodoma Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki SAMWEL SITA amesema ili kufikia mkakati huo wananchi hawana budi kuchangamkia fursa za kiuchumi za Shirikisho la Afrika Mashariki na kuachana na dhana kwamba soko hilo lipo kwa ajili ya wageni tu.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa SITA amesema Jumuiya hiyo imeshakamilisha maandalizi ya wimbo wa jumuiya hiyo tayari kuidhinishwa na wakuu wa nchi za Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages