Kamanada wa Polisi wa
mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen akionyesha gamba lisilopenywa risasi
lililonusuru maisha ya polisi wake katika mapambanao na majambazi katika
pori la Goma, barabara ya manyoni-Singida nje kidogo ya mji wa Dodoma,
wiki iliyopita. katika tukio hilo watuhumiwa wanne wa ujambazi waliuawa
na polisi
Wananchi wakijaribu
kunyanyua ili kujua uzito wa gamba lisilopenya risasi ambalo lilinurusu
maisha ya polisi yaliokuwa wakipambana na majambazi wa kurushiana risasi
katika msitu wa Goama, nje kidogo ya mji wa Dodoma wiki iliyopita.
Kamanda wa Polisi wa mkoa
wa Dodoma, Zelothe Stephen akionyesha bunduki iliyotengenezwa kienyeji
inayosadikiwa walikamatwa nayo watuhumiwa wanne wa ujambazi waliouawa
mjini humo wiki iliyopita katika majibishano ya risasi na polisi nje
kidogo ya mji wa Dodoma.
wananchi wakipanga foleni
kuingia chumba cha maiti cha hospitali ya mjini Dodoma kutambua maiti
za watu wanne waliouawa na polisi katika majibishano ya risasi
wakituhumiwa kwa ujambazi wa kuteka mabasi katika barabara kuu ya
Manyoni-Singida.
Wananchi watazama maiti
za watuhumiwa wa ujambazi iliyowekwa katika chumba cha maiti hospitali
ya mkoa wa Dodoma
Kamanda wa Polisi mkoa wa
Dodoma Zelothe Stephen na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk James Nsekela na
Mganga Mkuu wa hospitali ya Dodoma, Dk. Godfrey Mtei wakitoka katika
chumba cha maiti kwenye hospitali hiyo (Picha zote na Emmanuel Ndege
aliyekuwa Dodoma)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)