Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Bungo ya mkoani
Morogoro,akisimamia mtihani leo asubuhi.Wanafunzi wakiendelea na mtihani huo.
wengine wakitafakari na kufikili kwa umakini
KATIKA hali isiyo ya
kawaida, wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bungo ya mkoani Morogoro, leo asubuhi
walinaswa na mtandao huu wakiwa wametapakaa kwenye uwanja wa mpira wakifanya
mtihani huku wakiwa chini ya uangalizi mkali wa mwalimu wao.
Alipohojiwa na mwanidshi wa mtando huu juu ya wanafunzi hao kufanya mtihani kwenye uwanja huo, mwalimu aliyejitambulisha kwa jina moja la Mazinda, alisema uongozi wa shule hiyo uliwapeleka wanafunzi hao kufanya mtihani huo uwanjani hapo kwa lengo la kuwapa nafasi ili wasiangaliane majibu.
"Tumeamua wafanye mtihani huu wa majaribio hapa kiwanjani kwa lengo la kuwapa uhuru zaidi kwani pale darasani huwa wanabanana, lakini sambamba na hilo, hali hii itasadia kwa wale wanafunzi wenye tabia ya kunakiri majibu kutoka kwa wenzao washindwe kufanya hivyo," alisema mwalimu huyo kwa kujiamini.
Hata hivyo, mwandishi wetu alishuhudia wanafunzi hao wakifanya mtihani huo kwa shida kubwa kwani walilazimika kuinama kwa muda wote wakiwa hapo.

Habari Na Picha Kwa Hisani Ya DUNSTAN SHEKIDELE, /GPL, MOROGORO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)