Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es salaam
wamelilalamikia Shirika la Umeme nchini TANESCO kutokana na uwepo wa
tatizo la upatikanaji wa huduma ya Luku lililodumu siku ya nne sasa.
Wakizungumza na kituo hiki
baadhi ya wakazi hao wameelekeza tuhuma zao kwa watendaji wakuu wa
shirika hilo kwa kushindwa kulishughulikia tatizo lililopo hali
inayofanya wananchi waendelee kuishi katika hali ngumu ya kukosa umeme
hasa katika kipindi hiki cha sikukuu.
Kituo hiki kilipofika
Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam kupata
ufafanuzi kuhusiana na suala hilo mmoja ya wafanyakazi amesema watendaji
wakuu ambao ndio wasemaje walikuwa nje ya ofisi kushughulikia tatizo
hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)