Vunja vunja ya wanajeshi dhidi ya wanakijiji Kimbiji ! Polisi bado hawajaenda katika tukio - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Vunja vunja ya wanajeshi dhidi ya wanakijiji Kimbiji ! Polisi bado hawajaenda katika tukio

Uvamizi wa wanajeshi dhidi ya wanakijiji Kimbiji ! Polisi kigamboni wamekua BUBU!
hawajakubali kupokea malalamiko ya wanakijiji ! nani ? wa  kumfunga simba kengele?

MALI NA MAKAZI YA WANAKIJIJI WAPATAO 200 Kimbiji zimeharibiwa


Uvamizi uliofanyika 16.08.2011 jumatano saa 4.00 hasubui wakazi kijiji cha Kimbiji,nje kidogo ya jiji la Dar,
wamekuwa na mashaka ya maisha baada ya makazi na mazao yao kuharibiwa
vibaya na wanajeshi (JWTZ) ambao walivamia kijiji hiko na kuvunja vunja
makazi ya raia..kinyume cha sheria.
Hata hivyo baadhi ya wanakijiji walipereka taarifa katika vya  vituo vya polisi vya Kigamboni na mji mwema,havijakubali kupokea malalamiko ya wanachi walioharibiwa mali zao na kutishiwa
usalama wao,hadi sasa inaonekana kuwa wanachi wa Kimbiji hawana wa kuwalinda wao na mali
zao,kama inavyoeleza katiba ya nchi kuwa kila raia ana haki ya kupewa ulinzi wa maisha yake
na mali zake!

Katika Sakata hili la wanajeshi (JWTZ) kuvamia makazi ya raia na kuharibu mali za raia
bado lina utata  wa nani ? kumfunga kengengele simba?

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages