Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Regina Lowasa pamoja na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha Namelok Sokoine wakicheza mziki wa Kwaito na Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakati wa tafrija maalum ya kuwakaribisha warembo hao katika mji wa Monduli juzi mkoani Arusha. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Mke
wa Waziri Mkuu Mstaafu, Regina Lowasa akicheza mziki wa Kwaito na
Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakati wa
tafrijka maalum ya kuwakaribisha warembo hao katika mji wa Monduli juzi
mkoani Arusha. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini
kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Baadhi
ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa
wamevalia vazi maalum livaliwalo na wanawake wa jamii ya Kimasaai wakati
warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha
jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini
kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Warembo
wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakipakua chakula
wakati wa tafrija maalum ya kuwakaribisha katika mji wa Monduli jana.
Tafrija hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha,
Namelok Sokoine na dada wa Mbunge wa Monduli Kalaine Lowasa.
Warembo
wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika
picha ya pamoja na wenyeji wao baada ya kukaribishwa katika mji wa
Monduli jana katika tafrija iliyoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa
wa Arusha, Namelok Sokoine na dada wa Mbunge wa Monduli Kalaine Lowasa
Dada
wa Mbunge wa jimbo la Monduli na Waziri Mkuu mstaafu Kalaine Lowasa
akiwavisha warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011,
mgolole wa kimasai wakati warembo hao walipoandaliwa tafrija maalum ya
kuwakaribisha katika mji wa Monduli.Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum
Arusha, Namelok Sokoine. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea
vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine akimshika mkono mmoja wa
washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania baada ya kuvishwa
mgolole wa kimasai na dada wa Mbunge wa Monduli, Kalaine Lowasa (wapili
kushoto) jana baada ya kuwasili Monduli. Kushoto ni Mkurugenzi wa Lino
International Agency, waandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundenga
Baadhi
ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011,
wakiangalia nyoka aina ya chatu wakati warembo hao na wenzao
walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom
Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya
Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Mshiriki
wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, Glori Lori akiwa amejivisha
nyoka shingoni huku wenzake wakimwangalia wakati warembo hao na wenzao
walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom
Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya
Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Blessing
Ngowi, Mshiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, akiwa
amejivisha nyoka shingoni huku wenzake wakimwangalia wakati warembo hao
na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo
wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio
mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
===============================
Vodacom Miss Tanzania watembelea kaburi la Hayati Sokoine
Na Mwandishi Wetu
Ziara
ya mafunzo ya washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011
imeendelea Mikoa ya kanda ya Kaskazini na warembo hao wamepata fursa ya
kutembelea kaburi la aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe
Sokoine.
Wakiwa
eneo la Monduli warembo hao walipokelewa na Mtoto wa Sokoine Namelok
Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Arusha.
Mbunge
huyo alipata fursa ya kuwapa historia fupi ya maisha ya baba yake hasa
alipokuwa Waziri Mkuu,mapema walipowasili wilaya ya monduli walipokelewa
na mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Regina Lowasa na viongozi wengine wa
wilaya hiyo,Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Viti
Maalum wa mkoa wa Arusha Namelok Sokoine na alipata fursa ya kuwaasa
warembo hao pamoja na ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii na
maeneo ya kihistoria watumie fursa hiyo kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu
wa elimu kwa watoto wa kike hasa jamii ya kimasai,alisema jamii ya
kimasai ambayo inajishughulisha na ufugaji haijatoa kipaumbele katika
kumsomesha motto wa kike hivyo ziara ya warembo hao inaweza kutumika
kubadilisha mtizamo huo.
Akizungumzia
ziara hiyo Meneja Uhusiano na Habari kwa Njia ya Mtandao wa Vodacom
Tanzania Matina Nkurlu alisema washiriki hao walijifunza vitu mbalimbali
alivyovifanya Hayati Sokoine enzi za uhai wake.
Mara baada ya kutoka katika eneo hilo warembo hao 30 pia walitembelea shule ya Maasai Girls iliyopo Monduli kabla ya kupata chakula cha jioni.
“Ziara
yetu bado inaendelea na warembo wanaendelea kujifunza kupitia elimu
inayotolewa na wataalam mbalimbali wanaopata fursa ya kukutana na
warembo wetu. Ni matumaini yetu wataitumia elimu hii kulitangaza taifa
katika medani za kimataifa,” alisema Nkurlu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ndio waandaaji wa Vodacom
Miss Tanzania Hashim Lundenga alisema warembo hao pia watatembelea
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro NCAA, ili kujionea moja ya maajabu saba
ya dunia.
Akifafanua
Lundenga amesema mwaka huu wanataka warembo wenye sifa ikiwemo elimu,
muonekanao na tabia nzuri ili mshindi atakayepatikana aweze
kutuwakilisha vema katika medani za kimataifa hususani kujua vivutio vya
kitalii vilivyopo nchini.
“Baada
ya kutoka Mikumi ziara hii ya mafunzo sasa imeingia kanda ya kaskazini,
tukiwa safarini kutokea Morogoro warembo walipata fursa ya kupiga picha
katika maeneo mbalimbali ikiwemo daraja la mto wami na mji maarufu wa
Moshi mkoani Kilimanjaro,” alisema Lundenga.
Akizungumza
kwa niaba ya washiriki wengine mrembo Jennifer Kakolaki alisema kuwa
wanaifurahia ziara hiyo kwani mbali ya kujionea rasirimali tofauti
zilizopo nchini wanajifunza mengi kuhusiana na utalii wa ndani.
“Kiujumla
Watanzania hawana budi kutenga siku maalum katika mwaka ili kujionea
vivutio mbalimbali vilivyopo nchini. Binafsi nimepanua kiwango changu
cha ufahamu kuhusiana na utajiri wa rasilimali za taifa zilizopo
nchini,” alisema Jennifer.
Mwaka
huu warembo hao wameingia kambini kwa mfumo tofauti na uliozoeleka
kwani wamewekwa kwenye jumba maalum la ‘Vodacom House’ ambapo matukio
yao yatakuwa yakioneshwa kupitia Startv na Clouds TV na watazamaji
watapata fursa ya kupiga kura kuchagua mrembo watakayemuona anafaa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)