Meneja Masoko wa TWENDE,Hamis
Omary,akitoa maelezo kuhusiana na TWENDE,kulia Naomi Maro ,Mmoja wa
wajasiriamali,katika mkutano na waandishi wa Habari,Hadees Dar-es-
salaam,tarehe 18-8-2011
Meneja Mradi,Gloria Mongela,akitoa
maelezo kuhusiana na TWENDE,kulia Naomi Maro ,Mmoja wa
wajasiriamali,katika mkutano na waandishi wa Habari,Hadees Dar-es-
salaam,tarehe 18-8-2011
Naomi Maro,mmoja kati ya
wajasiriamali, kushoto ni meneja akitoa hoja kuhusu TWENDE,kushoto
akiwa na Meneja Masoko wa TWENDE, katika mkutano wa waandishi wa
habari, ulofanyika Hadees ,tarehe 18-august-2011
Naomi
Maro,mmoja kati ya wajasiriamali, kulia, akiwa na Meneja Mradi na
Meneja Masoko wa TWENDE wakijadiliana kuhusu TWENDE katika mkutano wa
waandishi na habari, ulofanyika Hadees ,tarehe 18-august-2011
----
Huu ni
mwaka wa pili wa TWENDE ambao utafanyika tarehe 15, 16 na 17 Septemba
mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar-es-salaam
Tunategemea
mahudhurio zaidi mwaka huu,katika hafla ya TWENDE kama njia ya
mawasiliano, kuendeleza na kuwahamasisha wanawake katika biashara zao
kitaifa na kimataifa alisema Gloria Mongela meneja mradi wa TWENDE.
TWENDE
imedhamiria kuchangia kutangaza malengo ya milenia ya 1,3,5 na 8,
ambayo ni kuondoa umasikini na njaa, kutangaza haki na fursa sawa kwa
wote, na kuwahamasisha wanawake kwenye afya zao na kuwaendeleza
uhusianao wa kudumu kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
”Ningependa
kusisitiza Uma kuhudhuria kwa kiasi kikubwa na kutumia fursa hii ya
TWENDE kuuendeleza ujuzi wakijisaliamali kwa kuuonyesha bidhaa na huduma
zao na pia kuhudhuria kwenye semina.Tunategemea ushirikiano mkubwa sio
tu kwa marafiki na familia bali kwa wanawake wote wajasiliamali na jamii
ya watanzania kwa ujumla”. Alisema Meneja Masoko wa TWENDE, Hamis Omary
Malengo
ya TWENDE ni kuwakuza kibiashara wajasiriamali wanawake nchini hii
itasaidia muongezeko wa wanawake wuzalishaji na uwiano sawa kibiashara
na kimasoko katika jamii iliyotawaliwa na Wanaume.
“
Tunaomba taasis za fedha ,maendeleo ya wanawake na watoo, na mashirika
yaliobobea katika maswala ya jinsia kushirikiana na TWENDE ili kuweza
kutimiza malengo ya Melenia namba 1,3,5 na 8, kwa kuwahamasisha wanawake
wajasililiamari, kuhudhuria maonesho na pia kusambaza taarifa kwa uma
kiujumla”,
aliongeza Mr.Omary.
Maonyesho
ya TWENDE, ni bure kwa watu wote ,ambapo yatafunguliwa saa 4:00 asubuhi
na kufungwa saa 12:00 jioni, kuanzia tarehe 15-17 Septemba 2011.
“Ninafurahia
TWENDE,kwasababu inatoa nafasi ya wajasiliamali kukutana na
kuwasiliana,na pia kupewa muunguzo mzuri katika biashara. Alsema Naomi
Maro,Mmoja kati ya wanawake wajasiriamali,walioudhulia,mkutano wa Twende
na waandishi wa habari.
Maonyesho
hayo ya siku tatu yataambatana na semina ili kuweza kuwapa
wajasiriamali wanawake mbinu za kuzishinda changamoto na kujiendeleza
kibiashara.
TWENDE
,imedhaminiwa na Daily News, Habari Leo, Perfect Machinery, Ultimate
Security, Global outdoor systems and 361 Degrees.
Ujumbe
wa TWENDE 2011:
Mimi Mwanamke, Mimi mjasiriamali
Hatanisipowezeshwa
nikiamua ninaweza
Mwanamke maendeleo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)