Taswira Za Muendelezo Wa Ziara Ya Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Huko Pemba - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taswira Za Muendelezo Wa Ziara Ya Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Huko Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,ALHaj Dk Ali Mohamed Shein,akiangalia mizani ya kupimia karafuu alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo katika kituo cha ununuzi wa karafuu cha Mkoani,Mkoa wa Kusini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,ALHaj Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Mtuhaliwa alipotembelea katika kambi ya wachumji wa karafuu katika eneo hilo,akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba,kutembelea mbali mbali za wachumaji wa zao hilo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,ALHaj Dk Ali Mohamed Shein,akielekeza jambo katika kituo cha ununuzi wa Karafuu cha MKoani Pemba alipofanya ziara ya kutembele kituo hicho na kuwakuta wananchi wakifanya usafi wa karafuu kabla ya kupimwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,ALHaj Dk Ali Mohamed Shein,akitembelea katika kambi ya wachumaji wa karafuu ya Ndugu Mohamed Khamis Ali Yussuf,Changaweni Mkoani Pemba,alipofanya ziara maalum ya kuona maendeleo za uchumaji wa zao hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,ALHaj Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba,baada ya kufutari nao katika futari aliyowaandalia wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Chake chake Pemba.(14/08/2011)
Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba,wakifutari kwa chakula walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Al Haj Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages