SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA APATA UGENI KUTOKA CHINA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA APATA UGENI KUTOKA CHINA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda(kushoto)akipokea zawadi kutoka kwa kiongozi wa ujumbe wa watu 12 kutoka nchini China, ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa The Chinese Political Consultative Conference(CPPCC), H.Z. Li Wuwei(kulia) katika ukumbi wa mikuatno wa ofisi za Bunge mjini Dodoma leo. Ujumbe huo uko nchini kwa ziara tangu Agosti 18,mwaka huu hadi Agosti21, mwaka huu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza na ujumbewa watu 12 kutoka nchini China, ukiongozwa na Makamu wa Mwenyekiti wa The Chinese Peoples Politicla Consultative Conference(CPPCC) , H.Z. Li Wuwei wa kwanza kutoka mstari wa mbele (kulia) na aliytupa kisogo kamera ni Naibu Spika Job, Ndugai katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Bunge leo mjini Dodoma. Ujumbe huo uko katika ziara ya hapa nchini tangu Agosti 18, mwaka huu hadi Agosti 21, mwaka huu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige akibonyenza kompyuta kwa ajili ya kupigia kura Mlima Kilimanjaro ili uwezwe kuingizwa kwenye shindano la maajabu saba ya asili ya Dunia kwa njia ya tovuti, katika ukumbi wa mikutano wa waandishi wa habari mjini Dodomaleo. Shindano hilo limeshaanza na litakamilika Novemba 11, mwaka 2011.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta(kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Msama Production, Alex Msama(kulia) katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma. 
Na Margreth Kinabo - MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages