Abiria
wa kwanza kusafiri na Precision Air kutoka Komoro walionekana kufurahia
huduma hiyo ya ndege. Jumla ya abiria walikuwa 110, ndege iliyofanya
safari hiyo ni aina ya Boeing 737-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 116.
Ndege aina ya Boeing 737-300 ilivyotua kwa mara ya kwanza uwanja wa ndege wa kimataifa wa Prince Ibrahim.
Mkurugenzi
Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse (kulia)
akikaribishwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi nchini
Komoro Bw. Abdulahi Mwinyi mara baada ya kuwasili na safari ya kwanza ya
shirka ya ndege hiyo kutokea uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere-Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko akiteta
na Mwenyekiti wa Galaxy General Sales Agents, Bw. Nassor Ali. Kampuni ya
Galaxy ni wakala rasmi wa Precision Air nchini Comoro.
.
Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse
Kioko akisindikizwa kwenda kupanda ndege na wenyeji wake baada ya
uzinduzi mfupi uliofanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Prince
Ibrahim, Hahaya-Komoro.
Afisa
Mawasiliano wa Precision Air, Bw. Amani Nkurlu akiwa na wana anga wa
shirika la ndege hilo walioshiriki kufanikisha safari ya kwanza ya
kwenda na kurudi Hahaya-Komoro kutokea Dar es Salaam jumatano iliyopita.
Habari Kwa Hisani Ya Father Kidevu Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)