Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Bw. Phil Mwakitawa
akizungumza katika hafla fupi iliokutanisha shirika la ndege hiyo na wadau wake
katika utangulizi wa kuzindua safari za Hahaya, Comoro na Johannesburg, Afrika
Kusini. Hafla hiyo ilifanyika Southern Sun Hotel jijini Dar es Salaam Ijumaa
iliyopita. Mkurugenzi huyo alisema kwamba wako tayari kupokea ndege yao mpya
aina ya Boeing 737-300 wiki hii kutoka Luton, London-Uingereza tayari kwa kuanza
safari za Comoro tarehe 17 na Johannesburg tarehe 24 mwezi huu wa
Agosti.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Meneja Mwendeshaji wa
Precision Air Bw. Allan Sharra (kulia) akizindua dansi baada ya kutoa hotuba
yake ilyoongelea ufanisi wa ndege yao mpya aina ya Boeing 737-300 itakayofika
wiki hii. Alisema ndege hiyo itaongeza idadi ya wasafiri kutoka 17,000 kwa wiki
hadi kufikia 70,000 kwa wiki.
Wadau wa Precision Air wakitoa 'cheers' kwa ishara ya
kuzindua safari za Hahaya na Johannesburg na kupokea ndege mpya ya Boeing
737-300.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Masoko wa Precision Air,
Bi. Elizabeth Mungwe (Kulia) akiwa na Meneja Mauzo Bw. Prosper Lawrence na Afisa
wa Mauzo Bi. Happiness Gachuma, wote kutoka The Citizen.
Mawakala mbali mbali wa usafirishaji wa anga pia
walikuwepo katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Precision Air
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)