Maafisa wa polisi wapatao 16,000 watafanya doria katika mitaa
ya London kudhibiti usiku wa nne wa ghasia mjini humo. Polisi wamesitisha likizo zao kuongeza nguvu kwa vikosi 30
Maduka na biashara katika baadhi ya maeneo yamefungwa kuepuka ghasia na
uporaji uliosambaa mjini London siku ya Jumatatu.Waziri Mkuu David Cameron ameahidi kurejesha hali ya utulivu, na Bunge litakutana Alhamisi kujadili ‘matukio ya kuchukiza’ ambayo yamesababisha vurugu pia katika miji mingine.
Polisi imetoa kile inachokiita ‘kitakuwa cha kwanza kwa picha za CCTV’ zinazoonyesha watuhumiwa wa ghasia hizo, huku watu 32 wakifikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi na uhalifu wa uliosababisha hasara wakati ghasia hizo zilpoanza.
Miongoni mwa watuhumiwa hao ni mbunifu wa michoro, wanafunzi wa vyuo, mfanyakazi wa vijana, kijana wa chuo kikuu na mtu mmoja aliyeandikishwa kuanza mafunzo ya kijeshi. Baadhi walitoa anwani ambazo si za London. Kumi na wanane walisalia rumande. Mpaka sasa watu 563 wamekamatwa na 105 wameshtakiwa kuhusiana na ghasia mjini London.
Naibu Kamishna Msaidizi wa Polisi Stephen Kavanagh alisema matumizi ya risasi za mpira-ambazo hayajawahi kutumika kabla kudhibiti ghasia England-yatatathminiwa kwa makini katika matukio mengine ya ghasia. Lakini aliongeza kuwa :"Hiyo haimaanishi kuwa tunaogopa kutumia mbinu nyingine yoyote." Kaimu Kamishna Tim Godwin alitupilia mbali ushauri wa kuliita jeshi
Source: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)