Mwanamama wa Uingereza Kizimbani Kutumikisha Binti wa Kitanzania - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mwanamama wa Uingereza Kizimbani Kutumikisha Binti wa Kitanzania


MWANAMAMA Mtafiti wa masuala ya kisayansi wa nchini Uingereza amebainika kumtumikisha binti wa kitanzania wa miaka 21 pasipo ujira wa aina yoyote ile kwa takribani nusu mwaka mzima.


Hayo yamefahamika jana asubuhi katika mahakama Southwark ambapo Mwanamama huyo Rebecca Balira anadaiwa kumtumikisha kimabavu binti Methodia Mathias kumpikia, kumwosha pia akimtumia kama yaya wa watoto wake watatu.

Binti huyo wa kitanzania aliingia mkenge huo baada kulaghaiwa na mama huyo kwamba angemlipa ujira wa pauni 96 kwa mwezi takribani Sh 300,000 za kitanzania, lakini hakuwahi kulipwa ujira huo katu. Majaji wameelezwa kuwa binti huyo amepokea kipigo mara kadhaa alipokuwa akihoji kuhusu ujira wake huo.

Mahakama pia imeelezwa kuwa binti huyo amenyang’anywa hati yake ya kusafiria na kupigwa marufuku kuwasiliana na ndugu na familia yake aliyoiacha Tanzania. Manyanyaso hayo yaliyodumu kwa miezi sita yalifikia kikomo baada ya binti huyo kufanikiwa kumweleza rafikiye ambaye alipiga simu Polisi na hatimaye suala hilo likaanza kuchunguzwa.
 
Kwa Habari zaidi waweza kubonya hapa Upate tukio hilo kwa kina.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages