Makamu
wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwahotubia wakazi wa Dodoma leo
wakati wa maadhimisho ya utekelezaji wa mwaka wa pili wa kauli ya
kilimo kwanza kwenye maadhimisho ya wakulima nanenane yanayoendelea
mjini Dodoma.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali ( wa tatu kutoka kulia) akipata
maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Pampu za kumwagiliaji aina ya Money
marker kwa mikoa ya Dodoma, Iringa na Ruvuma wa Kampuni ya Kick Start
International Deus Shauri( wa pili kulia) jinsi pampu hizo zilivyo
saidia kuinua kipato kwa baadhi ya wakulima wanaozitimika. Afisa huyo
alitoa maelezo hayo kwa Makamu wa Rais leo mjini Dodoma alioptembea
maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea.
Askari
wa kikosi cha kutuliza Ghasia mkoani Dodoma Anna Makenge(kushoto) na
Monica Haule(kulia)wakipata maelezo leo kutoka kwa Meneja Mawasiliano
wa Mfuko wa Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-T) Margaret Mussai juu
ya shughuli mbalimbali zinzosimamiwa na mfuko huo katika kuwaletea
maendeleo Watanzania. Polisi hao walipata maelezo hayo jana mjini
Dodoma wakati walioptembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho
ya wakulima nane nane yanayoendelea.
Mmoja wa watumishi wa umma wastaafu ambaye alikuwa Afisa Kilimo Mwandamzi Elias Sabuni akimuuliza Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma(kushoto) juu hatua za uboreshaji wa stahili za wastaafu mbalimbali katika Wizara mbalimbali. Mstaafu
huyo aliuza hayo leo mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya
Fedha kwenye maonyesho ya nane nane yanayoendelea m jinni Dodoma
Kitaifa.
Afisa Mikopo Mwandamizi wa Benki ya Uwekezaji Tanzania(Tanzania Investment Bank-TIB) Adelitha Kibuya akimweleza Makamu
wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali leo mjini Dodoma juu ya mikopo
mbalimbali inayotolewa na Benki hiyo katika kusiadia uwekezaji katika
sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wa wananchi. Afisa huyo alitoa
maelezo hayo jana mjini Dodoma wakati Makamu wa Rais alipotembelea
maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea Kitaifa mkoani hapa.
Afisa
Elimu Mazingira Mkuu kutoka Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais
Martha Ngalowera akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib
Bilali leo mjini Dodoma juu ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na
Ofisi hiyo katika kulielimisha jamii juu ya utunzaji mazingira kwa ajili
ya kizazi cha sasa na kijacho. Makamu wa Rais alitembelea maonyesho ya
wakulima ya nane nane yanayoendelea mjini Dodoma ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea.
Habari Kwa HIsani Ya John Bukuku - Full Shangwe Blogu





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)