MDAU HUMPHREY KATUTUMIA HII HAPA:TAHADHARI NA WEZI NDANI YA MABASI YA DAR EXPRESS - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MDAU HUMPHREY KATUTUMIA HII HAPA:TAHADHARI NA WEZI NDANI YA MABASI YA DAR EXPRESS

HABARI ZA LEO MDAU POLE NA MAJUKUMU YA KUJENGA TAIFA,KWANZA NATOA SHUKRANI ZA DHATI KUPATA NAFASI HII KUWAPA TAHADHARI WADAU WANAOTUMIA USAFIRI WA MABASI KWENDA MIKOANI. KUNA KAMPUNI MMOJA YA MABASI INAYOHESHIMIKA KWANZA KWA UBORA WABASI YAKE PAMOJA NA WAFANYAKAZI NADHIFU KAMPUNI HII INAITWA DAR EXPRESS, NI KAMPUNI YA SIKU NYINGI KATIKA NYANJA YA HUDUMA LAKINI HII KAMPUNI PAMOJA KUWA NA SIFA KEDEKEDE, INA DOA MOJA AMBALO WAHUSIKA WASIPOLISHUGHULIKIA ITAISHIA PAABAYA NA ITAPOTEZA WATEJA WAKE WENGI. PENGINE WATEJA WAO WANAWEZA KUHAMIA MAKAMPUNI KAMA KILIMANJARO EXPRESS,FRESH COACH,BUFFALO,SUMRY,METRO MAANA HATA MAKAMPUNI HAYO YANA MABASI YENYE STANDARD, NA HUDUMA SAFI. NISIELEZEE SANA DOSARI ILA NINAYO IZUNGUMZIA KUHUSU DAR EXPRESS NI WIZI AU UHALIFU UNAOFANYWA NDANI YA MABASI HAYA, MABASI YA DAR EXPRESS YANAYOELEKEA ARUSHA NA MOSHI YANAPOFIKA PALE HIGHWAY KOROGWE KWA AJILI YA CHAKULA, KUMEKUWA KUKITOKEA WIZI KWA ABIRIA MARA KWA MARA. JANA NINA RAFIKI YANGU ALIKUWA ANATOKEA DAR ANAKWENDA ARUSHA WALIPOFIKA PALE HIGHWAY WAKAENDA KULA AKAWA AMEACHA BEGI LAKE NDANI YA BASI KAMA KAWAIDA BEGI HILO LILIKUWA NA LINA LAPTOP. BAADA YA KURUDI KWENYE BASI LAPTOP ILIKWISHAKWAPULIWA NA MTU ASIYEJULIKANA, INASIKITISHA KWA KAMPUNI KAMA HIYO KUBWA INAKUWA INAPAKIA WEZI NA HUYO MWIZI UNAKUTA AMEKATA TIKETI VIZURI, AMEVAA VIZURI NA HUWEZI KUJUA. MWENZANGU AMESHARIPOTI POLISI NA POLISI NAO WANAKIRI WAMESHAPATA KESI NYNGI ZA NAMNA HIYO KUHUSIANA NA WIZI UNAOFANYIKA NDANI YA MAASI YA DAR EXPRESS. SIJUI HAO WAHUSIKA WA KAMPUNI YA DAR EXPRESS WAFANYAKAZI NA WAKURUGENZI WANACHUKULIA VIPI HILI SWALA AMBALO NI HATARI NA AIBU KUBWA KWA KAMPUNI KAMA HIYO IKIWA INAFANYA VITU KAMA HIVYO. INGEKUWA NI HAYA MA BUS MENGINE TUSINGE SHANGAA MAANA YANA BEBA WATU WA HADHI MBALI MBALI,LAKINI DAR EXPRESS INA DIGNITY YA KUBEBA WATU WA STATUS FULANI. SWALI LANGU KWA UONGOZI WA DAR EXPRESS WANCHUKULIA VIPI HII HALI NA HAO WALIOIBIWA MNA MPANGO GANI NAO?KWA KWELI NI AIBU DAR EXPRESS NARUDIA NI AIBU KUBWA SHAME ON YOU. THANKS

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages