Wakati
huu wa mfungo wa Ramadhani kumekuwa na mfumuko wa bei za vyakula katika
kila pembe ya nchi hii, na Zanzibar pia wananchi wamekuwa wakilalamikia
wafanyabiashara waliopandisha bei za vyakula hususan vile
vinavyotakikana zaidi wakati huu wa mfungo, kama Viazi, Mihogo, Nazi,
Tambi na vinginevyo.
Pichani
ni Roli lililosheheni magunia ya viazi likiingia maeneo ya katikati ya
mji wa Zanzibar ili kushusha bidhaa hiyo tayari kwa kuuza, kumbe si
kwamba upatikanaji wa vyakula umekuwa wa tabu la hasha bali ni
wafanyabiasha wenyewe tu walioamua kupandisha bei za vyakula kiholela
ili kujipatia faida kubwa kupitia mwezi huu.
Sehemu
ya mji wa Zanzibar unavyonekana nyumba zikiwa zimesongamana bila kuwa
na mpangiloa jambo ambalo ni hatari pindi inapotokea ajali ya moto na
nyinginezo, hapa ni mitaa ya Mlandege.
Picha Na Sufiani Mafoto







No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)