Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) William Lukuvi
(aliesimama) akisoma muongozo leo Bungeni mjini Dodoma, ((kulia) ni
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Mbunge
wa viti maalumu (CCM), Zainab Vullu akichangia Hotuba ya Makadirio ya
Matumizi ya Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kwa mwaka wa
Fedha 2011-2012 leo Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), John Mnyika akitaka ufafanuzi wa muongozo Bungeni Leo.
Mbungu
wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee (kushoto) akinyoosha mkono ili aweze
kupokelewa karatasi ya kuomba idhini ya Spika kuchangia hoja ya
majadiliano ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2011-2012 Bungeni mjini Dodoma
leo.Kulia ni Mbunge Owenya (CHADEMA) .
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge wa Viti Maalum, Faida
Bakari (kushoto) na Ritta Kabati kwenye viwanja vya Biunge Mjini
Dodoma leo.
Waziri
Mkuu,Mizengo Pinda akifurahia jambo na Katibu wa Jukwaa la wahariri
nchini,Neville Meena katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.
Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.
Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)