KIBAKA ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUPORA SIMU KATIKA KITUO CHA DALADALA CHA NANENANE MJINI DODOMA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KIBAKA ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUPORA SIMU KATIKA KITUO CHA DALADALA CHA NANENANE MJINI DODOMA LEO

Kijana Mmoja (wa katikati) Ambaye jina lake halikufahamika mara moja amenusurika kufa baada ya kupokea kipigo cha mbwa mwizi mara baada ya kupora simu ya mtasha mmoja ambaye alikua anaelekea katika maonyesho ya nanenane mjini dodoma leo.Kibaka Huyo alifanya tukio hilo wakati abiria wakiwa wanagombea daladala za kuelekea nanenane ambapo usafiri ulikua ni wa shida.
Hapa Raia wakiwa Wanamgombania Kibaka Huyo Kama Mpira Wa Kona kwaajili ya kumpa Kichapo huku askari wa usalama barabarani akijitahidi kumuondoa hapo ili ampeleke kituoni.
Askari Wa Usalama Barabarani Akimpa Mtasha(Mwenye Kapelo ya Kijivu) Simu yake iliyoporwa wakati akigombania daladala katika kituo cha daladala zielekeazo katika Viwanja Vya nanenane vilivyopo maeneo ya nzunguni
Askari Wa Usalama Barabarani akisaidiwa na Msamalia Mwema Kumkamata Kibaka vizuri ili kumpeleka kituo cha polisi kilichopo maeneo ya stand ya mkoa mjini dodoma mchana wa leo
Kibaka (Mbele) akiongozwa njia kwa kipigo cha wananchi huku akipelekwa Kituo cha polisi kwa ajili ya sheria kuchukua mkondo wake.
Raia wakiwa na uchungu wakutaka kuemdeleza kutoa kipigo kwa kibaka huyo huku askari wa usalama barabarani na msamalia mwema wakimshika vizuri asiwaponyoke na wakielekea kituo cha polisi.
Picha Zote na JOSEPHAT LUKAZA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages