HIVI ndivyo ilivyokuwa jinsi ilivyohifadhiwa
Mkuu
wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar SP Martin Lissu akizungumza na
waandishi wa habari katika eneo la tukio bandarini Zanzibar wakati wa
zoezi likiendelea.
Naibu
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar ACP. Muhud Mshihiri
akizungumza na wakala wa kusafirisha mizingi na msimamizi wa mzingo
huo, wakati wa zoezi la kuendelea kupekuwa magunia ya Dagaa ikiwa ndani
yake mmeweka Pembe za Tembo, kulia Kamanda wa Polisi Marine Zanzibar SP
Martin Lissu.
MMOJA
ya Konteni lilokuwa likisubiri kusafirishwa na kago ya magunia ya Dagaa
na kuchanganywa na Pembe za Tembo likiwa katika upekuzi baada ya
kugundulika kuwa na Nyara za Serikali zikitaka kusafirishwa nje ya
Nchi.
HIVI
ndivyo ilivyokuwa kufunguwa kila gunia kutowa kisicho husika katika
magunia ya Dagaa inayosemekana yakitokea Mwanza na kusafirishwa
nje kupitia bandari ya Zanzibar.
KIPUSA kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea katika bandari ya Zanzibar.
KIPUSA
kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea
katika bandari ya Zanzibar.Picha Zote na Mdau Othman Maulid--
Na Mwandishi wa MAELEZO-Zanzibar
Polisi Visiwani Zanzibar wamekamata Shehena kubwa ya Pembe za ndovu katika Bandari ya Malindi Visiwani hapa.
Hii ni Shehena
kubwa ya kwanza kukamatwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba ambapo
Polisi walifanikiwa kuigundua baada ya taarifa za Kiintelijensia
zilizofanyiwa kazi kitaalam.
Shehena hiyo ya Vipusa ilikuwa imepakiwa katika makontena mawili huku kukiwa na shehena ya samaki aina ya dagaa wa maji baridi.
Taarifa
ambazo bado hazijathibitishwa na Mamlaka husika, zinadai kuwa Shehena
hiyo ya Pembe za Ndovu ilikuwa ikipelekwa nchini Malaysia.Hadi saa 1:00
usiku Polisi walikuwa wakiendelea na kazi ya upakuaji na upekuzi zaidi
katika eneo la Bandari ambapo kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi
Bandarini,Martin Lissu watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano
zaidi.
Watu waliokamatwa ni pamoja na Wakala wa mizigo ambaye Polisi wamesema ni mapema mno kumtaja kwa sababu za kiupelelezi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)