Na Hamad Hija maelezo
Zanzibar
Waziri wa miundombinu wa Serikali ya mapindizi ya
Zanzibar Hamad Masuod Hamad, amezizinduwa rasmi kamati ya chuo cha mabaharia na
kamati ya safari usafiri wa anga ambazo zitasimamia uundwaji wa vyuo hivyo hapa
zanzibar.
Halfa ya uzinduzi wa kamati hizo ambazo zitakuwa na
majukumu ya kusimamia uanzishwaji wa vyuo hivyo imefanyika leo huko uwanja wa
ndege wa zamani huko kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akizitaja kamati hizo Waziri wa miundo mbinu na
mawasiliano Hamad Masuod Hamad, amewataja watakao unda kamati ya usafiri wa anga
kuwa ni pamojana Abdulla Hussein Kombo kuwa Mwenyekiti capteein Said mligati
,Said Suri na wengineo na kwa upande wa kamati ya anga wamo capteein Ali Haji
.Abdulrahman Chande, Engeneer Haji vuai Ussi pamoja na
Salma Suleiman omar
Amesema kuwa wamefikiria kuanzishwa kwa vyuo hivyo kwa
kuwa muda wa kufanya hivyo umefika kutokana na kuwa zanzibar kuna mabaharia
wengi,ambapo wengi wao wanafanya kazi ya ubaharia bila ya kuwa taaluma ya fani
hiyo.
Amsema kusudio la kuanzisha vyuo hivyo viwe vyuo
endelevu na vyenye hadhi ya vyuo ambapo watu wengi watapota nafasi ya kujifunza
hapa Zanzibar na sio viwe vyuo vya kienyeji
Aidha Masud amesisitiza kuwa, wanavyokusudia katika
uanzishwaji wa kamati hizo nikuona lengo la kuzipa uwezo wa kiutendaji hadi
kuanzishwa kwa vyuo hivyo hapa Zanzibar.
Aidha amefahamisha kuwa pamoja na kuanzisha kamati hizo
hivi sasa hakuna fungu la pesa ambazo zimetengwa kuendeshea lakini pesa za
kuendeshea shughuli hizo zitatoka katika taasisi husika ambazo zipo.
Akitaja kazi za kamati hizo ambazo zimezinduliwa leo
waziri huyo alisema kuwa miongoni mwa kazi zao ni pamoja na kuangalia kwa kina
utaratibu wa kuanzisha chuo cha ubaharia hapa Zanzibar pamoja na mfumo mzima wa
uendeshaji wa chuo hicho
Alisema kuwa pia kutakuwa na jukumu la kamati hizo
kuangalia kwa kina soko la chuo hicho hapa zanzibar na nje ya Zanzibar pamoja na
kutowa mapendekezo ju ya taratibu zitakazo tumika katika kutowa mafunzo katika
chuo
Aidha alitaja kuwa kazi nyengine zitakuwa kutowa na
kupendekeza mipango ya muda mrefu na muda mfupi ya kitaalamu ya uendeshaji
ambapo pia kutakuwa na majukumu ya kupendekeza taratibu za kutambuliwa chuo
hicho duniani.
Na kazi nyengine ambazo zimetajwa kuwa zitakuwa na
jukumu kubwa la kuorodhesha wataalamu waliopo hapa Zanzibar ambao watatumika
katika kuendesha mafunzo ya vitendo na nadharia
Picha Na Habari Kwa Hisani Ya John Bukuku - Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)