Watoa huduma wakibeba
mwili wa mtu mmoja kati ya watatu waliokutwa chumba Namba 425 kwenye
Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam leo.
Mwili wa aliyefariki ukipakizwa katika gari.
Imeelezwa kuwa mtu huyo
aliyekutwa amekufa ni raia kutoka Zambia, ambaye inadaiwa kuwa kifo chake ni
kunywa pombe kupita kiasi, huku wenzake wawili wakikutwa hoi na kupelekwa
Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu.
Aidha imeelezwa kuwa watu hao
wote mbao ni wanaume wamekutwa katika Chumba hicho kilichopo Ghrofa ya nne,
ambacho kilikuwa kimekodishwa na raia wa Uingereza.
Akizungumzia tukio hilo,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema kuwa mpaka sasa
hawajaweza kubaini undani wa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa tukio hilo
bado unaendelea.
Mmoja kati ya watu hao
aliyepata fahamu akiwa katika Hospitali yaMuhimbili ni Raia wa Uingereza,
aliyejitambulisha kwa jina la Eliud Sikwabi, aliyewataja wenzake kuwa ni Ikbar
Bahabur, ambaye ni raia wa Zambia pamoja na Mtanzania aliyetajwa kwa jina moja
la Omar.
Imeelezwa kuwa watu hao walikuwa ni miongoni mwa wageni waliokuwa wamehudhuria katika Harusi ya Mtoto wa Mark Bomani, Clement, ambapo walianza kupombeka katika sherehe hiyo na hatimaye wakaendeleza funda jingine baada ya kufika hotelini hapo.
Picha na
Stori hii ni kwa Hisani ya Blog ya Michuzi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)