Mbunge wa Singida mjini,Mohamed Dewji akizungumza na
walimu wa shule za sekondari jimbo la Singida mjini ili kuinua taaluma
itakayowawezesha wanafunzi kuondokana na aibu ya matokeo mabaya ya mtihani wa
kidato cha pili na ule wa kidato cha nne wakati alipokutana nao mwishoni mwa
wiki.
Makamu mwenyekiti wa manispaa ya Singida na diwani wa
kata ya Mitunduruni,Pantaleo Sorogai,akisalimia walimu wa sekondari za manispaa
ya Singida.
Afisa elimu wa sekondari manispaa ya Singida,Magreth
Mafita akitoa taarifa yake kwa mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Dewji
(mwenye shati la kijani) mwishoni mwa wiki.Wa kwanza kushoto,Meya wa
manispaa,Sheikh Salum Mahami na kulia kaimu mkurugenzi wa manispaa ya
Singida,Mzee Hoja.
walimu wa shule za sekondari za manispaa ya Singida
wakifuatilia mkutano huo.
Na.Mwandishi wetu,Singida.
Walimu wa shule za sekondari jimbo la Singida mjini,
wamehimizwa kukaza ‘buti’ katika kutekeleza wajibu wao, ili kuinua taaluma
itakayowawezesha wanafunzi kuondokana na aibu ya matokeo mabaya ya mtihani wa
kidato cha pili na ule wa kidato cha nne.
Changamoto hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na mbunge
wa jimbo hilo, Mohammed Gullam Dewji, wakati akizungumza kwenye kikao cha pamoja
na walimu wa shule 20 za sekondari za manispaa ya Singida.
Aliwaomba waendelee na moyo wao huo wa kujituma kwenye
kazi yao ya ufundishaji, ili kunyanyua ufaulu wa wanafunzi.
“Taarifa nilizo nazo, hali ya ufaulu kwenye shule zetu
iko chini mno, ni imani yangu kuwa baada ya kikao chetu hiki, morari na juhudi
za ufundishaji mtaziendeleza kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi”
alifafanua.
Aidha, Dewji ambaye pia ni mjumbe wa MNEC wa mkoa wa
Singida,aliwataka waendelee kuwa wavumilivu wakati huu ambao serikali inaendelea
kutatua changamoto nyingi zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu
yao.
“Changamoto mlizoziwasilisha kwangu, tutajipanga mimi
na viongozi wenzangu tuone ni kwa jinsi gani tunaweza kuzitatua zile zilizo
ndani ya uwezo wetu, na zile ambazo ziko nje ya uwezo wetu, tutaziwalisha
serikalini kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa kudumu”,alisema.
Awali afisa elimu wa shule za sekondari katika manispaa
ya Singida, Magreth Mafita, alitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili ofisi
yake, kuwa ni kucheleweshwa kulipwa kwa madai ya walimu na uhaba mkubwa wa
walimu.
Mafita alitaja changamoto zingine kuwa ni uhaba wa
vyumba vya madarasa, shule mpya kutokuwa na barabara za kuziunganisha na sehemu
zingine na ufaulu usioridhisha wa asilimia 42.
“Hata hivyo, mheshimiwa mbunge naomba nitumie fursa hii
kukupongeza sana kwa juhudi zako za dhati zilizopelekea jimbo la Singida mjini,
kuwa na shule za sekondari za serikali 17 kati ya mbili zilizokuwepo mwaka
2005”,alisema afisa huyo na kushangiliwa kwa nguvu na umati wa
walimu.Picha na Mbeya Yetu Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)