Chuo kikuu chafungwa Swaziland - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Chuo kikuu chafungwa Swaziland

Mfalme Mswati III
Chuo kikuu cha Swaziland hakijafunguliwa kwa mwaka mpya wa masomo baada ya serikali kushindwa kutoa fedha za ada za wanafunzi.
Chuo hicho kimetangaza kuwa hatua ya kusajili imesimamishwa na masomo kuahirishwa.
Kiongozi wa jumuiya ya wanafunzi Pasika Dlamini alisema wanafunzi wengi hawakuhudhuria masomo baada ya tangazo hilo.
Nchi hiyo ina upungufu mkubwa wa fedha kiasi ambacho wiki iliyopita Afrika Kusini iliamua kuwapa mkopo wa dharura wa dola za kimarekani milioni 355.
Chuo hicho kimeithibitishia BBC kwamba, kwa kuwa fedha bado hazijafika kuwalipia ada wengi wa wanafunzi hao, hakikuweza kufunguliwa.
" Tuliambiwa kuwa chuo hakitafunguliwa siku ya Jumatatu, kwasababu hamna pesa, " alisema Bw Dlamini.
Mwaka huu serikali ilisema itawafadhili takriban wanafunzi 300, kiwango kilichopungua sana ukilinganisha na wanafunzi 1,200 mwaka jana.
Mapato ya Swaziland ya mwaka jana kutoka ushuru wa forodha wa kusini mwa Afrika- chanzo kikuu cha fedha nchini humo- kilishuka kwa asilimia 60.
Baada ya kukubaliana na mkopo, Afrika Kusini ilisistiza jirani yake mdogo lazima ifanye mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa.
Mfalme Mswati III, mfalme pekee barani Afrika mwenye mamlaka kamili, ameshutumiwa kwa kuishi kwa ufahari na wake zake 13, huku watu wake wengi wakibaki maskini.
Pia kumekuwa na ripoti kuwa nchi hiyo, ambayo ina waathiriwa wengi wa virusi vya ukimwi dunaini, imepungukiwa na dawa za kufubaza ukimwi za ARV.
Source: BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages